Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Local News Wafanyikazi wa hospitali ya rufaa ya Isiolo walalamika kwa kutolipwa

Wafanyikazi wa hospitali ya rufaa ya Isiolo walalamika kwa kutolipwa

Baadhi ya wafanyakazi katika hospitali ya rufaa ya isiolo wanalilia haki, wakidai kuwa hawajapokea mshahara kwa kipindi cha miezi sita.

Kulingana na wafanyakazi hao, hali hiyo imewapelekea kupitia changamoto ikiwemo kulipa karo, kupata lishe na vile vile kulipa kodi ya nyumba huku ikiwalazimu wengi wao kutafuta njia mbadala za kujikimu kimaisha. Kitendo ambacho limekashifiwa na baadhi ya viongozi na vile vile wanaharakati wa kutetea haki za binadamu.

Akizungumuza mjini Isiolo mwaharakati Ibrahim wako amekashifu kitendo hicho na akaiomba serikali ya kaunti kuwalipa wafanyakazi hao kabla ya mwaka wa kifedha 2020/2021 kufungwa ifikapo tarehe 30 mwezi huu.

Ni kauli imbayo imeungwa mkono na seneta wa Isiolo Fatuma Dullo, akisema kwamba wafanyakazi wengi wa vibarua, vile vile hawajalipwa kwa muda mrefu. Hata hivyo juhudi za redio shahidi  kuwatafuta washikadau husika katika sekta ya afya jimboni kuhusiana na madai hayo zimeambulia patupu.

Wakati uo huo, Katibu mkuu wa muungano wa kitaifa wa madaktari na wataalam wa meno KMPDU Devji Atella amezitaka srikali za kaunti humu nchini kuwalipa madaktari mishahara yao na kusema kuwa madaktari wanapitia wakati mgumu kimaisha kwani hawajaweza kulipwa kwa muda mrefu sasa.

Devji amesema kuwa serikali za kaunti zimekuwa zikiichelewesha mishahara ya madaktari na wahudumu wengine wa afya huku wafanyakazi wengine wakipata mishahara.

Hapo awali serikali za kaunti zililalamikia ukosefu wa pesa za kuendeleza shughuli za serikali na kusema kuwa iwapo serikali ya kitaifa haitoziachailia pesa inazodaiwa na serikali za kaunti basi shughuli za serikali hizo zitaweza kusimamishwa.

RELATED ARTICLES

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Mwanaume apatikana ameuwawa eneo la Redcross

Hali ya woga imetanda katika eneo la Redcross wadi ya Bullapesa,kaunti ya Isiolo, hii ni baada ya mwili wa mwanamume mmoja mwenye...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Readings at Mass Tuesday 7 September 2021

23rd Sunday in Ordinary Time  Liturgical Colour: Green. First reading Colossians 2:6-15

Blessed Frederic Antoine Ozanam

7TH SEPT Antoine-Frederic Ozanam was an ordinary guy with extraordinary talent who lived an ordinary life but loved in...