WAKAAZI WAPUUZA MIKAKATI YA WIZARA YA AFYA

0
161

Zaidi ya watu kumi wamepoteza maisha yao kutokana na maambukizi ya virusi vya corona katika kaunti ya Isiolo tangu kuripotiwa kwa kisa cha kwanza cha corona nchini.

Waziri wa afya wa kaunti ya Isiolo, Bw.Wario Galma amesema kuwa  zaidi ya watu mia mbili hamsini wamepatikana na virusi vya corona katika kaunti hii.

Haya yanajiri huku baadhi ya wakaazi wakionekana kupuuza mikakati iliyowekwa kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo, ambao unaendelea kulemaza maisha ya maelfu nchini.

Jumbe kutokana kwa watu wa nia njema zinaendelea kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii, wakishauri wakaazi kuwa watiifu, ushauri ambao unaendelea kluambulia patupu kwani wachache ndio wanaonekana kuvalia barakoa haswa kwenye maeneo ya umma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here