Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Local News Makamanda Wa Polisi Isiolo Wapata Mafunzo Ya Kuhakikisha Mijengo Jimboni Inafuata Kanuni...

Makamanda Wa Polisi Isiolo Wapata Mafunzo Ya Kuhakikisha Mijengo Jimboni Inafuata Kanuni Hitajika

Maafisa wa polisi katika kaunti ya Isiolo wakiongozwa na kamanda joseph kigen wamehamashishwa kuhusiana na jukumu lao katika kuhakikisha majengo yote katika kaunti hii yanafuata mikakati iliyowekwa na mamlaka ya ujenzi nchini NCA.

Ni mafunzo ambayo yametolewa na mamlaka hiyo ikishirikiana na kitengo cha kukabiliana na majanga nchini katika ukumbi wa police mess mjini Isiolo.

Akizugumuza na wanahabari mjini Isiolo, mkurugenzi mkuu wa kitengo cha kukabiliana na majanga nchini amesema kwamba majengo yote yanayoendelea jimboni yanastahili kuwa yamesajiliwa kwa kitengo hicho ili kuhakikisha yanajengwa ipasavyo.

Aidha, Susan Ruto ambaye ni meneja mkuu kwenye mamlaka ya ujenzi nchini amedokeza kuwa wanakadarasi wengi wamekuwa na mazoea ya kuendeleza majengo yasiyofuata kanuni zinazohitajika huku akisisitiza kuwa ushirikiano wao na idara ya usalama utahakikisha kuwa wamekomesha jambo hilo.

Aidha mkurugenzi mkuu wa kitengo cha kukabiliana na majanga nchini Dkt. Dancan Ochieng amenukuu kuwa kuna umuhimu wa kusajili majengo yanayoendelea katika kaunti hii kwenye kitengo hicho kama njia mojawapo ya kuhakikisha wanazingatia kanuni hitajika.

Kumekuwepo na ongezeko la visa vya majumba kuporomoka nchini kutokana na baadhi ya wanakandarasi kukaidi kanuni zinazohitajika katika ujenzi.

Kuporomoka kwa majumba kunatokana na kuwekwa kwa misingi dhaifu, kutumia nyenzo zisizo imara katika ujenzi, wafanyikazi kufanya makosa, jengo kuwa nzito kuliko inavyohitajika na udhabiti wa jengo kutofanyiwa majaribio.

RELATED ARTICLES

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Mwanaume apatikana ameuwawa eneo la Redcross

Hali ya woga imetanda katika eneo la Redcross wadi ya Bullapesa,kaunti ya Isiolo, hii ni baada ya mwili wa mwanamume mmoja mwenye...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Readings at Mass Tuesday 7 September 2021

23rd Sunday in Ordinary Time  Liturgical Colour: Green. First reading Colossians 2:6-15

Blessed Frederic Antoine Ozanam

7TH SEPT Antoine-Frederic Ozanam was an ordinary guy with extraordinary talent who lived an ordinary life but loved in...