Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News National News MWANAUME ANAYEDAIWA KUWATEKA NYARA NA KUUWA WATOTO 10 AKAMATWA NAIROBI

MWANAUME ANAYEDAIWA KUWATEKA NYARA NA KUUWA WATOTO 10 AKAMATWA NAIROBI

Makachero wa uchunguzi wa jinai DCI wanamzuilia mwanaumwe mwenye umri wa miaka 20 anayeshukiwa kuwateka nyara na kuwaua watoto mjini Nairobi.

Masten Milimu Wanjala amekiri kuuwa watoto wawili wa miaka 13 na 12 ambao waliripotiwa kuwa wamepotea mnamo tarehe 30 juni na tarehe 7 julai mtawalia katika mtaa wa shauri moyo jijini Nairobi.

Kwa mujibu wa polisi, mwanaume huyo alikuwa amewapigia simu wazazi wa watoto hao na kuwaamuru wamtumie pesa ili awaachilie wanao.

Kwenye kisa cha kwanza, alimpigia mamaye mtoto na kudai shilingi elfu hamsini kutoka kwake. Vilevile kulingana na DCI Wanjala alimpigia baba ya mtoto wa pili na kumwamuru amtumie shilingi elfu thelathini ili amwachilie mwanaye.

Wanjala aliwaongoza wapelelezi hadi kwenye eneo ambalo alitekeleza uhuni huo. Inadaiwa kwamba Wanjala aliwateka nyara watoto hao walipokuwa wanaelekea nyumbani kutoka shule ya msingi ya Sagaret iliyoko katika eneo la Majengo.

Idara ya DCI inaamini kwamba mshukiwa huyo amehusika na vifo vya watoto kumi.

RELATED ARTICLES

RAIS KENYATTA AANDAA MKUTANO BAINA YA RAILA NA VINARA WA ONE KENYA

Rais Uhuru Kenyatta leo amekutana na viongozi watano wa vyama vya kisiasa humu nchini. Ni mkutano ambao umekisiwa wa kujaribu kuwaunganisha Raila...

KAUNTI ZOTE ZIWE NA MAHAKAMA KUU, ASEMA JAJI MKUU

Jaji mkuu Martha Koome amesisitiza haja ya kaunti zote nchini kuwa na mahakama kuu. Koome ameiambia baraza la magavana kwamba majimbo saba...

IEBC yawahoji watakao jaza nafasi za makamishna.

Tume ya mipaka na uchaguzi(IEBC) inaendeleza shugli  ya  kuwapiga msasa  watu 35 walioteuliwa kujaza nafasi ya makamishna wanne waliojiuzulu kutoka kwa...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Readings at Mass Tuesday 7 September 2021

23rd Sunday in Ordinary Time  Liturgical Colour: Green. First reading Colossians 2:6-15

Blessed Frederic Antoine Ozanam

7TH SEPT Antoine-Frederic Ozanam was an ordinary guy with extraordinary talent who lived an ordinary life but loved in...