Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Local News Serikali ya Marsabit Yaitelekeza zahanati ya Toricha iliyojengwa na kusalia magofu

Serikali ya Marsabit Yaitelekeza zahanati ya Toricha iliyojengwa na kusalia magofu

Wakaazi wa eneo la Toricha katika wadi ya Maikona, wamelalamikia kusahaulika n ahata kutelekezwa na serikali ya kaunti ya Marsabit.

Wenyeji hao wakiszungumza na Radio Jangwani wanasema kwamba zahanati ilijengwa katika eneo hilo miaka mitano iliyopita ila kufikia sasa hawajaona matunda yoyote ya zahanati hiyo.

Ndani Mwa Zahanati Ya Toricha, Iliyobaki Mahame.
Picha; Silvio Nangori.

Wanasema kuwa sasa wanalazimika kutembea kilomita takriban 60 kutoka eneo hilo hadi Maikona jkutafuta huduma ya matibabu licha ya kuwa na jingo lililolengwa kuwa zahanati.

Aidha wameifichulia Jangwani kuwa serikali ya kaunti ya Marsabit ilimwajiri muuguzi kuhudumu katika zahanati hiyo ila tangu kuajiriwa kwake hajawahi kanyaga katika eneo hilo.

Wenyeji ambao wamegubikwa na hasira kwa kukosa huduma ya afya wamekiri kuwa kinamama na watoto wadogo wanapougua wanapelekwa hadi eneo la maikona kupata matibabu.

Aidha Chifu wa Eneo hilo Ibrae Jaldesa akiongea na Shajara ya jangwani kwa njia simu, ameweka wazi kuwa ni ukweli zahanati hiyo imekuwa na muuguzi licha yake kutokanyanga eneo hilo hadi sasa.

Chifu  huyo ameshikilia dawa zilizotengewa zahanati hiyo pamoja na muuguzi  zimekwama Maikona licha ya waakazi  hao kung’ang’ana na hali tete ya maisha.

RELATED ARTICLES

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Mwanaume apatikana ameuwawa eneo la Redcross

Hali ya woga imetanda katika eneo la Redcross wadi ya Bullapesa,kaunti ya Isiolo, hii ni baada ya mwili wa mwanamume mmoja mwenye...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Readings at Mass Tuesday 7 September 2021

23rd Sunday in Ordinary Time  Liturgical Colour: Green. First reading Colossians 2:6-15

Blessed Frederic Antoine Ozanam

7TH SEPT Antoine-Frederic Ozanam was an ordinary guy with extraordinary talent who lived an ordinary life but loved in...