Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Local News SERIKALI YA ISIOLO YAZINDUA CHANJO YA POLIO KWA AWAMU YA PILI

SERIKALI YA ISIOLO YAZINDUA CHANJO YA POLIO KWA AWAMU YA PILI

Serikali ya kaunti ya isiolo imezindua zoezi la kuwachanja watoto walio chini ya miaka mitano dhidi ya ugonjwa wa polio hapo kesho.

Serikali za kaunti 13 zinazopakana na kaunti za Garrisa na Mombasa zimeombwa kuanzisha mpango wa kuwachanja watoto, baada ya visa vya polio kuanza kushuhudiwa katika maeneo hayo.

Waziri wa afya katika kaunti ya Isiolo Wario Galma amesema kuwa zoezi hilo linatarajiwa kuendelea kwa siku tano kuanzia hapo kesho jumamosi, shughuli ambayo itahakikisha kuwa kila mtoto anapata chanjo. Galma vilevile amesema kuwa chanjo hiyo inapeanwa bila malipo.

“Ningependa kuwahimiza wazazi wawapeleke watoto wao wapate chanjo ya polio kuanzia hapo kesho, itaendelea kwa siku tano, ugonjwa ya kupooza ni mbaya sana na hakuna mzazi angependa mtoto wake ashindwe kutembea”

Vile vile Galma amewaomba wazazi kujitokeza na kuwapeleka watoto wao kwenye vituo vya afya ili waweze kupata chanjo, semi ambazo zimeungwa mkono na chifu wa eneo la Waso james chuchu.

Wawili hawa wamezungumza na redio shahidi hii leo walipokuwa kwenye hafla ya uzinduzi wa shughuli hiyo katika hospitali ndogo ya waso.

Aidha Galma amesema kuwa wananchi hasa wazazi wasiskize dhana potovu kuhusu chanjo hio ya polio

“Kuna propaganda inaenezwa ya kwamba hii chanjo imeongezwa virusi vya corona, kwa kweli wataalam na wafanyakazi na wataalam wanawahakikishia hakuna virusi vimeekwa kwa hii chanjo na ukweli ni kwamba chanjo ya corona haipewi watoto wa chini ya miaka 18 kwa hivyo haiwezekani watoto wa miaka 5 kupewa chanjo ya corona”

RELATED ARTICLES

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Mwanaume apatikana ameuwawa eneo la Redcross

Hali ya woga imetanda katika eneo la Redcross wadi ya Bullapesa,kaunti ya Isiolo, hii ni baada ya mwili wa mwanamume mmoja mwenye...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Readings at Mass Tuesday 7 September 2021

23rd Sunday in Ordinary Time  Liturgical Colour: Green. First reading Colossians 2:6-15

Blessed Frederic Antoine Ozanam

7TH SEPT Antoine-Frederic Ozanam was an ordinary guy with extraordinary talent who lived an ordinary life but loved in...