Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Local News CHANJO YA POLIO KUENDELEA HADI ALHAMISI, BAADA YA IDD

CHANJO YA POLIO KUENDELEA HADI ALHAMISI, BAADA YA IDD

Washikadau katika sekta ya afya na wale wanaohusika katika vita dhidi ya maradhi ya polio wametangza kuwa zoezi la upeanaji wa chanjo ambalo limeingia siku ya tatu hii leo litaendelea hadi siku ya alhamisi baada ya sherehe za Idd.

Akizungumza na Radio shahidi balozi wa vita dhidi ya polio katika kaunti ya isiolo Mohhammed Abdulahi amesema kuwa kwa sasa zoezi hilo linaendelea kama inavyoratibiwa. Aidha Abdulahi amesema kuwa wazazi wasifikiri kuwa zoezi hilo limefikia kikomo hii leo.

“kwa sababu ya sherehe za Idd-ul-adha kesho, zoezi hili limeahirishwa. Lakini ningependa kuwaomba wazazi watayarishe watoto wao kwa chanjo hiyo siku ya Alhamisi,” Abdulahi amesisitiza

Waziri wa usalama na mambo ya ndani ya nchi Dkt Fred Matiang’i wiki jana alitangaza jumanne tarehe 20 Julai kuwa sikukuu ya kitaifa, kuadhimisha sherehe za kiislam za Idd-ul-adha.

Vile vile Abdulahi ameeleza kuwa kwa sasa lengo lao ni kuhakikisha kuwa asilimia 100 ya watoto walio chini ya miaka mitano wanapata chanjo ikilinganishwa na asilimia 98 ya awamu iliopita ya zoezi hilo.

Upeanaji wa chanjo ya polio katika kaunti hii ya isiolo ulizinduliwa siku ya ijumaa katika hospitali ndogo ya waso baada ya kaunti 13 zilizo katika hatari ya kupata ugonjwa huo kuagizwa kuanzisha zoezi hilo.

RELATED ARTICLES

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Mwanaume apatikana ameuwawa eneo la Redcross

Hali ya woga imetanda katika eneo la Redcross wadi ya Bullapesa,kaunti ya Isiolo, hii ni baada ya mwili wa mwanamume mmoja mwenye...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Readings at Mass Tuesday 7 September 2021

23rd Sunday in Ordinary Time  Liturgical Colour: Green. First reading Colossians 2:6-15

Blessed Frederic Antoine Ozanam

7TH SEPT Antoine-Frederic Ozanam was an ordinary guy with extraordinary talent who lived an ordinary life but loved in...