Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News National News KAUNTI ZOTE ZIWE NA MAHAKAMA KUU, ASEMA JAJI MKUU

KAUNTI ZOTE ZIWE NA MAHAKAMA KUU, ASEMA JAJI MKUU

Jaji mkuu Martha Koome amesisitiza haja ya kaunti zote nchini kuwa na mahakama kuu. Koome ameiambia baraza la magavana kwamba majimbo saba yaliyosalia bila mahakama kuu yanafaa kuzingatiwa.

Jaji mkuu anasema hii ni mojawapo ya jitihada za kuhakikisha kwamba haki inapatikana kwenye maeneo yote ya taifa la Kenya, ili kufanikisha marekebisho ya idara mahakama ambayo yamekuwa yakitekelezwa kwa miaka 10 iliyopita.

Wakati uo huo, Koome amezitaka kaunti kubuni njia nyingine mbadala za kusuluhisha mizozo pasipo kushusisha mahakama yaani ADR, pamoja na kuanzisha vituo vya kulinda haki za watoto.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa baraza la magavana Martin Wambora, kaunti zinazosalia bila mahakama kuu ni pamoja na Samburu, Wajir, Mandera, Lamu, Elgeyo Marakwet, Nandi na Nyandarua.

Mwezi jana idara ya mahakama ilipata motisha mkubwa baada ya rais Uhuru Kenyatta kuapisha majaji 35 zaidi, jambo lililomfurahisha jaji mkuu katika siku zake za kwanza afisini.

Koome anaamini kwamba changamoto kuu la mrundiko wa kesi ulioko mahakamani kwa sasa litaweza kusuluhishwa iwapo mahakama zaidi zitajengwa kwenye maeno yote ya nchi.

RELATED ARTICLES

RAIS KENYATTA AANDAA MKUTANO BAINA YA RAILA NA VINARA WA ONE KENYA

Rais Uhuru Kenyatta leo amekutana na viongozi watano wa vyama vya kisiasa humu nchini. Ni mkutano ambao umekisiwa wa kujaribu kuwaunganisha Raila...

MWANAUME ANAYEDAIWA KUWATEKA NYARA NA KUUWA WATOTO 10 AKAMATWA NAIROBI

Makachero wa uchunguzi wa jinai DCI wanamzuilia mwanaumwe mwenye umri wa miaka 20 anayeshukiwa kuwateka nyara na kuwaua watoto mjini Nairobi.

IEBC yawahoji watakao jaza nafasi za makamishna.

Tume ya mipaka na uchaguzi(IEBC) inaendeleza shugli  ya  kuwapiga msasa  watu 35 walioteuliwa kujaza nafasi ya makamishna wanne waliojiuzulu kutoka kwa...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Readings at Mass Tuesday 7 September 2021

23rd Sunday in Ordinary Time  Liturgical Colour: Green. First reading Colossians 2:6-15

Blessed Frederic Antoine Ozanam

7TH SEPT Antoine-Frederic Ozanam was an ordinary guy with extraordinary talent who lived an ordinary life but loved in...