Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Church News ASKOFU MUKOBO AONYA DHIDI YA KUHAIRISHA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2022

ASKOFU MUKOBO AONYA DHIDI YA KUHAIRISHA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2022

Kanisa limeendelea kuhimiza umuhimu wa kura ya maoni kufanyika baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 na si kabla. Akiongea wakati wa ibada ya jumapili kwenye kanisa la Mt. Eusebius mjini Isiolo, Askofu wa jimbo katoliki la Isiolo Anthony Ireri Mukobo ametoa mwito kwa viongozi kuiheshimu katiba ya sasa.

Askofu Ireri amesema kwamba hakuna haja yoyote ya kuahirisha uchaguzi kwa sababu ya kura ya maoni kupitia mswada wa BBI. Amesema kwamba kuahirisha uchaguzi huenda kukasababisha hali ya sintofahamu ya kisiasa nchini au uwezekano wa kuvuruga Amani.

Askofu Ireri amesisitiza ujumbe uliosomwa na baraza la maaskofu wakatoliki nchini KCCB mwezi Mei kuhusu kura ya maoni na uchaguzi, ambao ulihimiza viongozi kuhubiri jumbe za Amani na kuheshimu katiba ya mwaka 2010.

Kauli ya askofu Ireri imejiri wakati mahakama ya rufaa ikitarajiwa tarehe 20 mwezi ujao kutoa uamuzi kuhusu mswada wa marekebisho ya katiba mwaka 2020. Uamuzi huo utabaini iwapo Kenya itakuwa na kura ya maoni au la.

Ikumbukwe kwamba baada ya taarifa ya pamoja ya maaskofu iliyotolewa mwezi Mei, rais Uhuru Kenyatta aliitika wito wao na kuwaapisha majaji waliokuwa wameteuliwa na tume ya JSC.

RELATED ARTICLES

SHANGWE ZARINDIMA SHEREHE ZA MTAKATIFU EUSEBIUS ISIOLO

Na Tracy Nakato Parokia ya  mt. eusebius, jumapili imesherehekea siku kuu ya familia ambayo imemsherehekea mtakatifu Eusebius. Mtakatifu Eusebius...

REMEMBERING LUIGI LOCATI, FIRST BISHOP OF ISIOLO

At the geographical heart of Kenya, below the scorching sun of the northern   part of Kenya, stands the twin rectangular towers, that...

KANISA KATOLIKI LASISITIZA HAJA YA VIONGOZI KUHESHIMU SHERIA

Kanisa limeendelea kusisitiza haja ya viongozi na asasi za serikali kuheshimu sheria. Ni maafikio yaliyotangazwa na maaskofu wa kanisa katoliki nchini Kenya...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Readings at Mass Tuesday 7 September 2021

23rd Sunday in Ordinary Time  Liturgical Colour: Green. First reading Colossians 2:6-15

Blessed Frederic Antoine Ozanam

7TH SEPT Antoine-Frederic Ozanam was an ordinary guy with extraordinary talent who lived an ordinary life but loved in...