NYOTA YA MATUMAINI KWA VIJANA WANAOITAJI KUJIKIMU NA KOZI ZA KIUFUNDI

0
296
Baadhi ya vijana waliofaidika kupitia mpango wa Ujuzi Manyattani ulioanzishwa na shirika La NRT

Huku Kenya ikizidi kufanikisha ruwaza ya mwaka wa elfu mbili na thelathini, vijana wanazidi kutakiwa kujikimu na ujuzi wa kiteknikali ili waweze kupata nafasi za ajira kupitia miradi ya serikali.

Mojawapo ya miradi iliyoanzishwa ili kuwapa vijana mafunzo haya, ni mradi wa Ujuzi Manyattani, ulioanzishwa na shirika la Northen Ragelands trust, kwa ushirikiano na hifadhi za jamii na shule ya mafunzo ya kiufundi ya  Kiirua training Institute.

Kulingana na Tom Lalampaa, ambaye ndiye mkurugenzi mkuu wa NRT, mpango huu unanuiwa kuwafikia vijana katika viwango vya vijiji, ikikumbukwa kuwa mtindo wa maisha ya wafugaji ni kuhama kutoka eneo moja hadi lingine kwa minajili ya kuwatafutia mifugo wao lishe.

Katika warsha uliofanyika katika hifadhi ya jamii ya kalama, na kuongozwa na  katibu mkuu wa viuo vya kiufundi Dkt. Margraet Mwakima,  wanafunzi mia moja hamsini walihitimu. Kulingana na  Dkt. Magrete,  serikali inazidi kuzipa usaidizi gatuzi za kaunti ili kuinua Zaidi masomo ya vyuo vya kuifundi.

Juhudi hizi kutoka kwa serikali na vile vile mashirika husika ni kwa kupelekea kuwapa vijana ujuzi wa kujiajiri ili waweze kujikimu kimaisha. Kulingana na ripoti ya ajira nchini, Zaidi ya vijana millioni tano ambao ni asilimia kumi na moja nukta nne  hawana ajira.

Vijana milioni nane, elfu mia nne thelathini na sita elfu mia nne kumi na wanane hawana ajira. Kati ya idadi hii,  vijana millioni moja, laki sita arubaini na saba elfu, mia nne themanini na wanne wangali wanatafuta kazi, huku vijana millioni tatu laki tano elfu arubaini wakiwa bado hawajaingia kabisa katika soko la kazi.

Ata hivyo swala hili, kupitia  juhudi baina ya washikadau mbalimbali nchini linatarajiwa kusuluhishwa.

Tangu uanzilishi wa mpango wa Ujuzi Manyattani mwaka wa elfu mbili kumi na tisa, vijana mia mbili na tisa wamehitimu, ambayo ni asilimia tisini na saba ya vijana elfu mbili kumi na wanne ya waliojisajili. Kwa miaka minne ijayo, mpango huu unatarajiwa kuwafaidi Zaidi ya vijana elfu tano, na kuwa na walimu mia tatu hamsini.  Mpango huo kufikia sasa unatoa kozi kumi na mbili, ambazo zinazidi kusomwa na wanafunzi kupitia vyuo vilivyo katika hifadhi zao.

Kando na kufunzwa bila karo, wanafunzi hawa wanafaidika kwa kupewa vyombo vya kuanzisha biashara za ujuzi wao. Mpango huu ukitarajiwa kupunguza kutoajiriwa baina ya vijana kwa kutokuwa na ujuzi unaohitajika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here