Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Church News SHANGWE ZARINDIMA SHEREHE ZA MTAKATIFU EUSEBIUS ISIOLO

SHANGWE ZARINDIMA SHEREHE ZA MTAKATIFU EUSEBIUS ISIOLO

Na Tracy Nakato

Parokia ya  mt. eusebius, jumapili imesherehekea siku kuu ya familia ambayo imemsherehekea mtakatifu Eusebius. Mtakatifu Eusebius wa Vercelli ndiye mlezi wa kanisa la cathedrali isiolo. Alizaliwa mwaka wa 282 baada ya kirstu Italia na kupata mafunzo yake ya upadri uko Roma kisha Kutawazwa askofu mwaka wa 340.

Mtakatifu Eusebius ambaye ndiye mtakatifu mlezi wa kathedrali ya Isiolo.

Sherehe hii ambayo hufanyika kila mwaka tarehe mbili mwezi wa Agosti, ilianza mwanzoni mwa wiki, ambapo wakristu walishiriki kwa sala na kupewa mafunzo kutokana na maisha ya mtakatifu huyo.

Akizungumza kuhusu siku hii baba paroko wa kathedrali ya jimbo katoliki la Isiolo, James mureithi amesema kuwa kupitia mtakatifu Eusebius, kanisa hili liliweza kueneza huduma na injili kwa wakaazi katika mji wa isiolo.

Fr. James Mureithi ambaye ndiye baba paroko wa Jimbo Katoliki la mt.Eusebius akiwahutubia waumini.

Wakristu pia nao wameeleza furaha yao kusherehekea siku hii wakisema kuwa ni ya maana.

Aidha vikundi mbali mbali vilijumuika Pamoja ili kuidhinisha siku hii ambayo ilikuwa yenye furaha, shangwe na nderemo.

Baadhi ya vikundi vilivyoudhuria kuadhimishwa kwa siku hii, vimesema kuwa vinazidi kuiga mfano wake mt. Eusebius katika kueneza injili.

Baadhi ya kina mama wa CWA walio saidia kufanikisha siku hii.

Katika mechi iliyofanyika katika uwanja wa shule ya Hekima, vijana walikishindia kikombe katika mchezo wa kambumbu na mbio.

Kikundi cha vijana wanaofanya kazi (YCW) walishinda mchezo wa voliboli, na vile vile kikundi cha waimbaaji (choir)  wakipata kikombe kutokana na kushirikiana kwao katika kuinua hali ya litujia kanisani.

Vijana wa kathedrali baada ya kuibuka bingwa katika mchezo wa kabumbu na kutuzwa kwa kikombe.

PICHA ZAIDI ZA WARSHA HUU, ZITACHAPISHWA KATIKA UKURASA WETU WA FACEBOOK TAREHE 11-08-2021

RELATED ARTICLES

ASKOFU MUKOBO AONYA DHIDI YA KUHAIRISHA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2022

Kanisa limeendelea kuhimiza umuhimu wa kura ya maoni kufanyika baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 na si kabla. Akiongea wakati wa...

REMEMBERING LUIGI LOCATI, FIRST BISHOP OF ISIOLO

At the geographical heart of Kenya, below the scorching sun of the northern   part of Kenya, stands the twin rectangular towers, that...

KANISA KATOLIKI LASISITIZA HAJA YA VIONGOZI KUHESHIMU SHERIA

Kanisa limeendelea kusisitiza haja ya viongozi na asasi za serikali kuheshimu sheria. Ni maafikio yaliyotangazwa na maaskofu wa kanisa katoliki nchini Kenya...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Readings at Mass Tuesday 7 September 2021

23rd Sunday in Ordinary Time  Liturgical Colour: Green. First reading Colossians 2:6-15

Blessed Frederic Antoine Ozanam

7TH SEPT Antoine-Frederic Ozanam was an ordinary guy with extraordinary talent who lived an ordinary life but loved in...