Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News National News RAIS KENYATTA AANDAA MKUTANO BAINA YA RAILA NA VINARA WA ONE KENYA

RAIS KENYATTA AANDAA MKUTANO BAINA YA RAILA NA VINARA WA ONE KENYA

Rais Uhuru Kenyatta leo amekutana na viongozi watano wa vyama vya kisiasa humu nchini. Ni mkutano ambao umekisiwa wa kujaribu kuwaunganisha Raila Odinga wa ODM, na wenzake wanne kutoka muungano wa One Kenya.

Mwelekeo huu umeonekana kama njia mojawapo ya kutafuta mwelekeo wa siasa za urais mwakani, kwenye mkutano uliowaleta pamoja Kalonzo Musyoka wa WIPER, Musalia Mudavadi (ANC), Moses Wetangula wa FORD Kenya na kiongozi wa chama cha KANU Gideon Moi.

Hata hivyo taarifa kutoka ikulu ya rais haijaweka wazi iwapo maswala ya siasa yamejadiliwa kwenye mkutano huo. Msemaji wa ikulu ya rais Kanze Dena amesema kwamba nia ya mkutano huo ilikuwa ni kutathmini hali ya taifa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo aidha, viongozi hao wamejadili janga la Covid 19 nchini, na jinsi ya kufufua uchumu. Kadhalika mkutano huo pia umenuiwa kudumisha Amani, umoja na uwiano wa taifa nchini.

Mkutano huu umejiri baada ya uliokuwa muungano wa NASA kusambaratika ambapo Odinga, Kalonzo, Mudavadi na Wetangula walikuwa wadau.

RELATED ARTICLES

Heshima za Mwisho, huku rais Kenyatta akimuomboleza Charles Njonjo

Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu na waziri Charles Mugane Njonjo ameaga dunia. Kifo chake kilitangazwa jumapili...

POLISI WATALINDA WANAHABARI WAKATI WA UCHAGUZI, ASEMA INSPEKTA MKUU

Idara ya polisi itajizatiti kuhakikisha usalama kwa waandishi wa habari nchini, hasa wakati huu taifa linapoelekea kwenye uchaguzi mkuu mwakani. Hii ndiyo...

SIKU YA KIMATAIFA KUKOMESHA DHULUMA DHIDI YA WANAHABARI YAADHIMISHWA

Mkurugenzi wa mashtaka ya uma DPP Noordin Haji jumanne aliwahakikishia wanahabari kwamba watalindwa vya kutosha dhidi ya vitisho...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

St. Emilie de Vialar

18th January St. Emilie de Vialar (Emily) was born in 1797 in Gaillac and ancient town in the south...

Readings at Mass Tuesday 18 January 2022

Second Week in Ordinary Time  Liturgical Colour: Green. First reading 1 Samuel 16:1-13

WENYEKITI WA BODABODA ISIOLO KUSHIRIKIANA NA VITENGO VYA USALAMA ILI KUPELEKEA KUMALIZIKA KWA UHALIFU

Muungano wa wenyekiti wa wahudumu wa bodaboda Isiolo, umesema kushirikiana Pamoja na maafisa wa  kulinda usalama, ili kumaliza uhalifu katika kaunti hii....

Msako mkali wa pombe haramu wafanyika Isiolo.

Idara ya NGAO katika kaunti ya Isiolo wamefanya msako wa pombe haramu katika eneo la Bula Pesa katika kaunti hii.