Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Local News Wafanyikazi wa kuuza mchanga waandamana.

Wafanyikazi wa kuuza mchanga waandamana.

Zaidi ya wafanyikazi 400 wanaofanya kazi ya kuuza mchanga wa ujenzi katika kaunti ya Isiolo waliandamana mjini Isiolo kulalamikia ongezeko la kodi ambayo wamekuwa wakilipa kwa serikali ya kaunti ya Samburu na Isiolo.

Wakizungumza na wanahabari wafanyikazi hao walisema kuwa tangu kizuizi hicho kilipowekwa katika eneo la Ngaremara kaunti ya Isiolo wamekuwa wakilazimika kulipa kodi kwa kaunti ya Isiolo na Samburu.

”Tunapitia changamoto nyingi tangu kodi hiyo iongezwe hata hatuwezi kulipa wafanyikazi na tunashindwa kukimu maisha yetu na familia zetu’’  Alisema Ben Mugambi ambaye ndiye  mwenyekiti wa chama cha wafanyikazi hao.

Vile vile Monica Gikundi alilalamikia   kuharibika kwa bara bara kunakopelekea wao  kuwapoteza wenzao kufuatia utovu wa usalama kushudiwa maeneo hayo licha ya  kodi inayolipwa kwa  kaunti zote mbili.

Wafanyikazi hao sasa wameitaka serikali kuu kuingilia kati na kutatua changamoto wanazopitia na kusema  kuwa wamefanya mikutano na viongozi katika kaunti ila hakuna hatua iliyochukuliwa kufikia sasa.

RELATED ARTICLES

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Mwanaume apatikana ameuwawa eneo la Redcross

Hali ya woga imetanda katika eneo la Redcross wadi ya Bullapesa,kaunti ya Isiolo, hii ni baada ya mwili wa mwanamume mmoja mwenye...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Readings at Mass Tuesday 7 September 2021

23rd Sunday in Ordinary Time  Liturgical Colour: Green. First reading Colossians 2:6-15

Blessed Frederic Antoine Ozanam

7TH SEPT Antoine-Frederic Ozanam was an ordinary guy with extraordinary talent who lived an ordinary life but loved in...