Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Local News Msaada watolewa kwa waathiriwa wa ubomozi Mwangaza

Msaada watolewa kwa waathiriwa wa ubomozi Mwangaza

Waathiriwa wa ubomozi wa nyumba katika eneo la Mwangaza kaunti ya Isiolo,  wamepokea msaada wa vifaa vya ujenzi na vyakula kutoka kwa serikali ya kaunti.

Haya yanajiri siku chache  baada ya familia kadha  kubomolewa nyumba zao  asubuhi ya jumapili  iliyopita.

Akizungumza katika hafla hiyo afisa mkuu  wa mipango maalum katika kaunti ya Isiolo,  Abdia Dabaso-  alisema kwamba msaada huo ulitolewa na serikali ya kaunti kwa ushirikiano na shirika la msalaba Mwekundu. Vile vile alikashifu tukio hilo huku akiwaomba wakaazi kuwa watulivu huku sheria ikifuatiliwa.

Wakati uo huo, Dabaso aliwaomba wakaazi wa Mwangaza kuandaa kikao ili kutafuta suluhu la kudumu kwa njia ifaayo bila kuwahusisha wanasiasa.

Aidha kwa upande wao  wakaazi wa eneo hilo walishukuru kwa msaada ila wakaiomba serikali ya kaunti kuwatatulia tatizo hilo la ardhi kutokana na kukidhiri kwake katika eneo hilo. Kadhalika waliomba serikali ya kaunti kuwaachilia vijana waliokamatwa siku hiyo wakidai kuwa hawana hatia.

Aata hivyo kamishna wa kaunti ya Isiolo Geoffrey Omoding’ aliwataka wakaazi kuwa watulivu huku serikali ikitafuta suluhu, na kuwatahadharisha dhidi ya kujenga katika eneo linalozozaniwa hadi kesi itakapoamuliwa.

Kumekuwepo na mizozo ya ardhi katika eneo la Mwangaza ila  maswali yanayosalia  ni-  Je, kulikuwa na uhalali wa amri ya mahakama kuhusu ubomozi huo? Je suluhu la kudumu litapatikana kwa wakaazi wa eneo hilo?

RELATED ARTICLES

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Mwanaume apatikana ameuwawa eneo la Redcross

Hali ya woga imetanda katika eneo la Redcross wadi ya Bullapesa,kaunti ya Isiolo, hii ni baada ya mwili wa mwanamume mmoja mwenye...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Readings at Mass Tuesday 7 September 2021

23rd Sunday in Ordinary Time  Liturgical Colour: Green. First reading Colossians 2:6-15

Blessed Frederic Antoine Ozanam

7TH SEPT Antoine-Frederic Ozanam was an ordinary guy with extraordinary talent who lived an ordinary life but loved in...