Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Local News KAUNTI YA ISIOLO YAPIGA HATUA KWENYE ZOEZI LA KUWACHANJA WAKAAZI DHIDI YA...

KAUNTI YA ISIOLO YAPIGA HATUA KWENYE ZOEZI LA KUWACHANJA WAKAAZI DHIDI YA COVID-19

Huku serikali kuu ikiendeleza kampeni ya wananchi kujitokeza kupokea chanjo ya virusi vya corona, serikali ya kaunti ya Isiolo haijasalia nyuma kwenye mchakato huo.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na waziri wa afya katika kaunti ya Isiolo Wario Galma tayari watu 5,160 walikuwa wamepokea chanjo dhidi ya virusi Corona kufikia tarehe 24 Agosti 2021, huku wakaazi waliopokea dozi ya kwanza ya corona wakiwa ni 3,165.

Kulingana na takwimu zilizoonekana na Radio Shahidi, wananchi ambao hawajawekwa kwenye orodha ya wanaopewa kipaumbele kupokea chanjo wamejitokeza kwa wingi katika kaunti hii.

“Kati ya hao kina mama ni 1,046 na wanaume ni 2,119, wafanyikazi wa serikali wakiwa ni 325, walinda usalama 407 na walimu 264” Galma akasema

Waliopokea chanjo ya dozi ya pili ni watu 1,896, wengi miongoni mwao wakiwa ni walio na umri wa Zaidi ya miaka 58.

Wakati uo huo, wafanyikazi wa serikali walionekana kujitokeza kwa wingi kupokea dozi ya pili. Hii ni kufuatia makataa iliyotolewa na mkuu wa wafanyakazi wa umma Joseph Kinyua, iliyowaamuru wafanyakazi wote wa serikali kuchanjwa dhidi ya Covid 19 ifikapo tarehe 23 mwezi Agosti mwaka huu.

“Wafanyikazi wa serikali 240, walinda usalama 167, walimu ni 206, walio na umri Zaidi ya 58 wakiwa ni 644 na wananchi wasio kwenye orodha ya waliopewa kiapumbele kupokea chanjo ya virusi vya corona 589 wamepokea chanjo kaunti ya Isiolo.”

Kufikia tarehe 22 mwezi huu jumla ya watu 2,412,209 walikuwa wamepata chanjo ya Covid 19 nchini Kenya.

Hata hivyo, miongoni mwa hawa, Watu 1,631,022 ni waliopokea dozi ya kwanza pekee na 781,187 wakipokea dozi ya pili.

Kenya imepokea msaada wa dozi ya chanjo ya corona kutoka mataifa yanayojiweza ikiwemo uingereza na Marekani.

Kulingana na waziri wa afya nchini Kenya Daktari Mutahi Kagwe, Kufikia tarehe 21 mwezi huu kenya ilikuwa imepokea jumla ya dozi milioni 3.6 ya Astrazeneca na Moderna huku ikitarajia kupokea dozi milioni 4.5 ifikapo katikati mwa mwezi Septemba mwaka huu, “Lazima uzingate vigezo vya kupata maambukizi hata kama umepata chanjo.”

Licha ya idadi ya maambukizi kushuhudiwa kuongezeka siku baada ya siku, wakaazi wengi wa Isiolo wameonekana kulegeza Kamba.

Hadi kufikia jumanne tarehe 24 wiki hii, watu 482 waliripotiwa kuambukizwa virusi vya corona katika kaunti ya Isiolo. Hii ni kutokana na jumla ya sampuli 3,345 ambazo zilikuwa zimepimwa tangu kisa cha kwanza kuripotiwa nchini.

Idadi ya wanaume walioripotiwa kuambukizwa katika kaunti ya Isiolo ilikuwa ya juu kuliko hile ya wanawake. Kwa mujibu wa takwimu za wizara ya afya katika kaunti ya Isiolo tarehe 24 Agosti 2021, wanaume walioambukizwa ni 330, wakiwakilisha asilimia 68.46 na wanawake 152, wakiwakilisha asilimia 31.53.

Vile vile katika muda huo, watu 31 wamepoteza maisha yao kutokana na Covid 19. Kufikia tarehe 22 mwezi huu watu 13 walikuwa wamelazwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi kwenye hospitali ya rufaa ya Isiolo na wagonjwa wengine 23 wanaoendelea kuuguzwa nyumbani.

“Watu 415 wamepona kutokana na virusi vya corona… wahudumu wa afya 44 wakipata maambukizi ya virusi vya corona na wawili kupoteza maisha yao,” akaongeza Wario Galma

Kutokana na ongezoko la juu la maambukizi katika kaunti ya Isiolo na majirani zake, na vilevile kaunto zilizoko kaskazini na kaskazini mashariki mwa Kenya, viongozi wamewatahadharisha wananchi dhidi ya kulegeza Kamba.

Waziri wa afya kaunti ya Isiolo Wario Galma ametoa wito kwa wakaazi kuzingatia vigezo vilivyotolewa na wizara ya afya. Wakaazi vilevile, wamehimizwa kupokea chanjo pindi zitakapowasili, “Iwapo umeona dalili yoyote tafadhali fika hospitalini kwa matibabu kuzuia kusambaza kwa watu wengine”

Serikali inaazimia kuwachanja watu milioni 10 dhidi ya Covid 19 ifikapo mwezi Desemba mwaka huu, na wengine milioni 23 mwaka ujao.

Hata hivyo, kuna wasiwasi iwapo Kenya kama taifa ina uwezo wa kununua na kuhifadhi idadi kama hii ya chanjo.

RELATED ARTICLES

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Mwanaume apatikana ameuwawa eneo la Redcross

Hali ya woga imetanda katika eneo la Redcross wadi ya Bullapesa,kaunti ya Isiolo, hii ni baada ya mwili wa mwanamume mmoja mwenye...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Readings at Mass Tuesday 7 September 2021

23rd Sunday in Ordinary Time  Liturgical Colour: Green. First reading Colossians 2:6-15

Blessed Frederic Antoine Ozanam

7TH SEPT Antoine-Frederic Ozanam was an ordinary guy with extraordinary talent who lived an ordinary life but loved in...