Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Features MABILIONI YA KEMSA YAKO WAPI? UCHUNGUZI BUTU WA SERIKALI!

MABILIONI YA KEMSA YAKO WAPI? UCHUNGUZI BUTU WA SERIKALI!

Mwaka mmoja uliopita Rais Uhuru Kenyatta aliagiza uchunguzi kuanzishwa baada ya sakata ya wizi wa fedha kuikumba mamlaka ya usambazaji wa vifaa vya matibabu humu nchini KEMSA.

Hii leo mwaka mmoja baadae hakuna hatua yoyote ya kisheria ambayo imechukuliwa dhidi ya washukiwa. Sakata hii ilihusisha ufujaji wa zaidi ya billioni 7.8 kwenye shughuli za upeanaji wa zabuni na ununuzi na ufujaji wa fedha nyingine ambazo taifa la kenya lilipokea kama misaada ili kusaidia kwenye vita dhidi ya covid 19.

Uchunguzi wa wizi huu ulitakiwa kufanywa kwa awamu mbili, awamu ya kwanza ilihusisha kujua jinsi ambavyo millioni saba za ununuzi wa vifaa vya kujikinga vya madaktari wanapowahudumia wagonjwa wa covid 19 ulivyofanyika na waliohusika.

EACC pia ilitangaza kuwa ingalichunguza jinsi sheria ililivyokosa kufuatwa kwenye zoezi la upeanaji wa zabuni. Awamu ya pili ilihusisha kuzichunguza kampuni ambazo zilifanya biashara na KEMSA na jinsi ambavyo baadhi ya kampuni zilifaidika.

Kampuni moja iliwashangaza wengi baada ya kupewa kandarasi wiki moja tu baada yake kuanzishwa, Kampuni hio kwa jina Shop and Buy limited iliweza kupokea zaidi ya millioni kumi kutoka kwa KEMSA.

Ivy minyow Onyango aliisajili kampuni nyingine kwa jina Kilig Limited mwaka jana January 22 kabla ya kisa chochote cha covid 19 kuripotiwa humu nchini.

 Miezi miwili baadae kampuni yake iliweza kutunukiwa zaidi ya billioni 4 kwa kandarasi ya kusambaza vifaa vya kujikinga vya wahudumu wa afya.

Aidha inadaiwa kuwa kampuni hiyo ilisambaza vifaa hivyo kwa shillingi alfu tisa ambayo ilikuwa ni bei mara mbili zaidi ya bei ya kawaida. Inadaiwa kuwa kampuni yake haikuwa na vyeti kamili vya kupata kandarasi za kiasi kama hicho cha pesa.

Aidha pia uchunguzi mwingine ambao ungalifanywa ni uchunguzi wa kampuni ambazo ilidaiwa kuwa zilikuwa zinamilikiwa na baadhi ya wakuu serikalini ama wandani na jamaa zao, kampuni moja ilidaiwa kumilikiwa na gavana mmoja ambaye yuko madarakani kwa sasa. Kwa mfano kampuni ya Wallabis ventures ambayo ilipokea zaidi ya millioni 75 inadaiwa kumilikiwa na mmoja wa maafisa katika wizara ya afya.

Je, taifa la kenya lilipata matatizo gani kuhusiana na sakata hii?

Wizi wa pesa uliwapelekea madaktari kukosa vifaa muhimu vya kuwakinga wanapofanya kazi zao jambo ambalo liliwafanya zaidi ya madaktari alfu moja kupata virusi hivyo kwenye awamu ya kwanza ya maambukizi hayo.

Mwezi agosti mwaka jana wahudumu wa afya waliandaa mgomo wa kitaifa na kulalamikia kutolipwa marupurupu yao huku wakifanya kazi katika mazingira yasiyofaa.

Kwa wakati mmoja Waziri wa afya katika kaunti ya Machakos Daktari Ancent Kituku alisema kuwa vifo vingi vilivyoripotiwa katika awamu ya kwanza ya maambukizi ya covid 19 vilitokana na wagonjwa kukosa huduma bora ambazo zingeweza kupatikana iwapo pesa ambazo serikali ya kenya ilipokea zingetumika vizuri.

Je, viongozi wa KEMSA walisema nini kuhusiana na sakata hio nzima?

Aliyekuwa mkurugenzi mkuu mtendaji wa KEMSA Jonah Manjari alisema kuwa baadhi ya maamuzi aliyoyafanya yalitokana na maagizo ambayo alipokea kutoka kwa baadhi ya watu wakuu serikalini wakiwemo katibu mkuu na waziri katika wizara hiyo ya afya.

Mwenyekiti Kembi Gitura alikubali kuwa baadhi ya kandarasi zilizopeanwa hazikufuata sheria ila jambo hilo lilisukumwa na suala la covid 19 kuwa la dharura.

Je, serikali ya kenya ilifanya nini kuhusiana na suala hilo?

Tarehe 26 mwezi wa nane mwaka jana Rais Uhuru Kenyatta alitangaza kuwa ameipa tume ya maadili na kupambana na ufisadi siku 21 za kukamilisha uchunguzi, aidha EACC ilitangaza kuwa imewasilisha ripoti katika afisi ya DPP ili hatua zaidi za kisheria ziweze kuchukuliwa.

Kenya ilipokea shilingi billioni 78.3 kutoka kwa shirika la fedha duniani IMF, billioni 7.5 kutoka kwa umoja wa ulaya EU, billioni 108 kutoka kwa benki ya dunia na billioni 22.5 kutoka kwa benki ya maendeleo ya afrika chini ya siku sitini fedha ambazo zilikuwa za kusaidia vita dhidi ya covid 19.

Kwa sasa kenya imesajili visa 235, 299 vya covid 10 na vifo 4, 720 huku watu 222, 357 wakiweza kupona.

Yote haya yakionekana kuwekwa kwenye kikapu na kutupwa mvunguni mwa historia, wakenya wanasalia na maswali, je, Pesa zetu zilienda wapi? Na je, waliohusika katika ufujaji wa pesa kwenye mamlaka ya KEMSA ni kina nani na wako wapi?

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Readings at Mass Tuesday 7 September 2021

23rd Sunday in Ordinary Time  Liturgical Colour: Green. First reading Colossians 2:6-15

Blessed Frederic Antoine Ozanam

7TH SEPT Antoine-Frederic Ozanam was an ordinary guy with extraordinary talent who lived an ordinary life but loved in...