Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home Business Uwanja wa kimataifa wa ndege wa Isiolo kuanza kufanya kazi mwezi...

Uwanja wa kimataifa wa ndege wa Isiolo kuanza kufanya kazi mwezi Desemba.

Uwanja wa kimataifa wa ndege mjini Isiolo unatarajiwa kuanza kuanza kufanya kazi mnamo Desemba mwaka huu.

Hii ni baada ya Katibu wa wizara ya uchukuzi Simon Kitungu, mkurugenzi msimamizi wa mamlaka ya viwanja vya ndege (KAA) Alex Gitari na kitengo cha kuhakikisha miradi ya serikali kuu imekamilika PDU kuzuru kaunti ya Isiolo hii leo kukagua miradi inayoendelea kufanyika kwenye uwanja huo wa ndege.

Katibu wa wizara ya uchukuzi Simon Kitungu, mkurugenzi msimamizi wa mamlaka ya viwanja vya ndege (KAA) Alex Gitari na kitengo cha kuhakikisha miradi ya serikali kuu imekamilika PDU, baada ya kuwahutubia wanahabari kuhusiana na kukamilika kwa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Isiolo.

Baada ya kikao na gavana wa kaunti ya Isiolo Daktari Mohamed Kuti, katibu katika wizara ya uchukuzi Simon Kitungu amewahakikishia wakaazi kuwa uwanja wa ndege utakamilika mwezi Desemba mwaka huu. Kadhalika Kitungu ameeleza kuwa kwa kukamilika kwa ukarabati wa baadhi ya miradi katika uwanja huo wa ndege utaleta maendeleo katika kaunti ya Isiolo na Meru.

“Mkandarasi aliyepewa kazi katika uwanja wa kimataifa wa ndege Isiolo alifanya kazi mbovu na kutoroka lakini tunamalizia mchakato wa kumpata mkandarasi mwingine atakayefanya ukarabati wa uwanja huo kwa miezi miwili” Kitunguu asema

Mkurugenzi msimamizi wa mamlaka ya viwanja vya ndege (KAA) Alex Gitari alisema ujenzi wa eneo la kupakia mizigo tayari limekamilika kwa asilimia 55. Vile vile mkandarasi atakayehusika na kurekebisha barabara kuu ya uwanja wa ndege anatarajiwa kuanza kazi hivi karibuni. Barabara hiyo inatarajiwa kugharimu shilingi milioni 20

“Tumekuja kukagua miradi ya ujenzi wa pahala pa kupakia mizigo, ukarabati wa barabara kuu ya uwanja wa ndege ili uwanja huu uanze kufanya kazi.” Gitari asema

Kulingana na gavana Kuti amewahakikishia kuwa serikali ya kaunti na serikali kuu wanafanya kazi kwa pamoja kukamilisha ukarabati wa uwanja huo wa ndege ili uweze kuwafaidi wakaazi wa Isiolo pamoja na kaunti jirani kibiashara.

“Sisi tuko tayari kushirikiana na serikali kuu kwa vyovyote vile ili tuimarishe biashara katika kaunti hii na kaunti jirani” Kuti asema

Gavana Kuti akiwahutubia wanahabari nje ya makao makuu ya kaunti ya Isiolo.

Uwanja wa kimataifa wa ndege wa Isiolo ulifunguliwa rasmi tarehe 23 mwezi Agosti mwaka wa 2017. Hata hivyo kufuatia ukarabati wa baadhi ya miradi, uwanja huo haujaanza kufanya kazi. Pindi uwanja huo utakapoanza kufanya kazi unatarajia kusafirisha abiria 350,000 wanaofika na kuondoka kila mwaka.

RELATED ARTICLES

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Mwanaume apatikana ameuwawa eneo la Redcross

Hali ya woga imetanda katika eneo la Redcross wadi ya Bullapesa,kaunti ya Isiolo, hii ni baada ya mwili wa mwanamume mmoja mwenye...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Readings at Mass Tuesday 7 September 2021

23rd Sunday in Ordinary Time  Liturgical Colour: Green. First reading Colossians 2:6-15

Blessed Frederic Antoine Ozanam

7TH SEPT Antoine-Frederic Ozanam was an ordinary guy with extraordinary talent who lived an ordinary life but loved in...