Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Local News Mwanaume apatikana ameuwawa eneo la Redcross

Mwanaume apatikana ameuwawa eneo la Redcross

Hali ya woga imetanda katika eneo la Redcross wadi ya Bullapesa,kaunti ya Isiolo, hii ni baada ya mwili wa mwanamume mmoja mwenye umri wa makamo,  kupatikana nje ya lango la mkaazi.

Mwanaume huyo alikuwa na majeraha usoni, huku akisalia kuumizwa kwa kiwango cha kutotambulika kwa urahisi.

Kulingana na wakaazi wa eneo hilo, kulikuwa na mgurumo wa pikipiki eneo hilo usiku wa manane wa kuamkia jumatatu, jambo ambalo limewapelekea kuwaza kuwa mwanaume huyo aliuwawa eneo lingine kisha kutupwa hapo.

Vile vile kulingana na Hosea Kimathi, ambaye ndiye mwenye lango mtu huyo aliyetupwa nje yalo, aliiomba serikali kuimarisha usalama eneo hilo.

Asubuhi tumesekia watoto wakiongea walipokuwa wakienda shuleni wakisema kuna mtu ameuwawa, kuamka tukapata ametupwa kwa gate yetu. Area hii kumezidi sana- iko mtu aliuwawa akatupwa mater, ata miezi tano haijaisha, kwa hivyo tunaomba serikali kuongeza usalama.” Hosea alisema

Aidha, Kulingana na chifu wa lokisheni ya WASO, James Chuchu, maafisa wa polisi walifika hapo mapema kwa minajili ya kuuchukua mwili na vile vile kuanzisha uchunguzi.

Aidha,  Chifu Chuchu aliitaka serikali ya kaunti kushirikiana na serikali kuu ili kuimarisha usalama eneo hilo kwa kuweka taa.

Previous articleSt. Giles
Next articleBlessed Frederic Antoine Ozanam
RELATED ARTICLES

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Watu Kumi wakamatwa katika kaunti ya Isiolo na kufikishwa mahakamani

Watu kumi walikamatwa na maafisa wa polisi katika kaunti ya Isiolo na kufikishwa kwenye mahakama  ya isiolo. Kumi hao walishtakiwa kwa kosa...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Readings at Mass Tuesday 7 September 2021

23rd Sunday in Ordinary Time  Liturgical Colour: Green. First reading Colossians 2:6-15

Blessed Frederic Antoine Ozanam

7TH SEPT Antoine-Frederic Ozanam was an ordinary guy with extraordinary talent who lived an ordinary life but loved in...