Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Local News Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu...

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya Kambi ya Juu.

Baadhi ya madawati yaliyotolewa na redio shahidi kwa ushirikiano na mashabiki kwa shule ya msingi ya Kambi ya Juu

Akizungumza kwenye hafla ya kupokea dawati hizo mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Kambi ya Juu Jeniffer Makero amewashukuru wahisani waliowatunuku kwa madawati.

Ata hivyo, amewaomba wafadhili Zaidi kujitokeza kuwasadia, akisema shule hiyo ina changamoto kadha kwani inasomesha pia wanafunzi wenye ulemevavu.

“Tunashukuru kituo cha radio Shahidi kwa kuanzisha mpango huu na Mungu abariki kila mmoja aliyehusika kwenye mchango huo. Tunaomba usaidizi zaidi kutoka kwa wafadhili ili wanafunzi wawe na mazingira bora.” Makero asema

mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Kambi ya Juu Jeniffer Makero akiwashukuru wahisani waliowatunuku kwa madawati.

Aidha msimamizi wa mashabiki waliosaidia kufanikisha mpango huo Adesh tall ameshukuru Radio shahidi kwa kuanzisha mpango huo na kuwashukuru viongozi na mashabiki waliohusika.

“Shukrani nyingi ziwaendee viongozi,mashabiki kwa kuhusika kununua dawati hizi na tutaendelea kusaidia mahali ambapo palipo na pengo ili wanafunzi wetu wasome kwenye mazingira mema.” Adesh Asema

Adesh Tall akimkabidhi Mwalimu mkuu Jennifer madawati

Akiwasilisha ujumbe wa mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Isiolo, mwakilishi kutoka tume ya kuwaajiri walimu TSC Frankline Munene amewahimiza wanafunzi kutia fora na kuhakikisha wamezingatia mikakati ya kupambana na virusi vya corona.

“Usaidizi ambao umeletwa hapa hii leo ni wa kuhakikisha kuwa mnakaa kwa mazingira mema ya masomo, hivyo basi tunarajia alama nzuri kutoka kwenu wanafunzi.” Munene asema

Munene ametoa ahadi kwamba wizara ya elimu itahakikisha wamefuatilia uharibifu uliofanyika katika shule hiyo haraka iwezekanavyo ili masomo yaendelee vizuri.

“Tumewasilisha barua kwa serikali ya kaunti kulipa uharibifu uliofanyika katika shule hii wakati watoto wanaorandaranda mitaani walipoletwa hapa lakini kufikia sasa hakuna hatua iliyochukuliwa.

Wizara ya elimu itafuatilia jambo ili kuhakikisha vifaa vilivyoharibiwa vimetengenezwa.”

Kwa upande wake mkurugenzi wa idara ya mawasiliano katika Jimbo katoliki la Isiolo padre Simon Githaiga ametoa wito kwa washikadau tofauti kuhusika kwenye sekta ya elimu ili wanafunzi wawe na mazingira mazuri ya masomo.

Mkurugenzi wa Redio Shahidi padre Simon Githaiga, akiwashukuru wote waliofanikisha mpango huo.

“Ukipata elimu umeondoa wizi, vita, umeleta Amani na uwiano na kituo cha Radio Shahidi kinasaidia vile iwezavyo kuwasaidia wanyonge. Ni jukumu la washikadau tofauti, wizara ya elimu na serikali ya kaunti kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira bora ya elimu kwani watoto ndio viongozi wa kesho.” Githaiga asema

Radio Shahidi ingependa kuwashukuru wote waliofanikisha mpango huo, Sen. Fatuma Dullo, Sen. Abshiro Halake, Molla Illere, MCA Stella, Mwenda Thuranira, Karani(Waso Choma Zone), councillor Mugambi, na mashabiki wote.

RELATED ARTICLES

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Mwanaume apatikana ameuwawa eneo la Redcross

Hali ya woga imetanda katika eneo la Redcross wadi ya Bullapesa,kaunti ya Isiolo, hii ni baada ya mwili wa mwanamume mmoja mwenye...

Watu Kumi wakamatwa katika kaunti ya Isiolo na kufikishwa mahakamani

Watu kumi walikamatwa na maafisa wa polisi katika kaunti ya Isiolo na kufikishwa kwenye mahakama  ya isiolo. Kumi hao walishtakiwa kwa kosa...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

HOSPITALI YA AVI-MATERCARE YAPOKEA VIFAA VYA KUJIKINGA NA COVID 19

Hospitali ya AVI Matercare kaunti ya Isiolo Ijumaa wiki hii imepokea ufadhili wa vifaa vya kujikinga kutokana na maambukizi ya COVID 19...

TRUE, Poultry farming supports over 160 households in Uasin Gishu County

A Facebook post claiming that poultry farming supports over 160 households in Uasin Gishu county is true based on a study conducted...

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...