Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News HOSPITALI YA AVI-MATERCARE YAPOKEA VIFAA VYA KUJIKINGA NA COVID 19

HOSPITALI YA AVI-MATERCARE YAPOKEA VIFAA VYA KUJIKINGA NA COVID 19

Hospitali ya AVI Matercare kaunti ya Isiolo Ijumaa wiki hii imepokea ufadhili wa vifaa vya kujikinga kutokana na maambukizi ya COVID 19 kutoka benki ya Equity.

Akizungumza katika hafla ya kupokeza rasmi vifaa hivyo kwenye hospitali hiyo, Meneja wa oparisheni za banki hiyo ya Equity katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa nchi Bw.Hassan Maalim amesema kuwa lengo kuu la kupeana vifaa hivyo ni kuhakikisha kuwa wameisaidia jamii kwenye vita dhidi virusi vya corona.

“Bodi ya benki ya Equity iliamua kuanza mpango wa kusaidia hospitali za kidini kwa kuwapa vifaa vya kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona ili wawe salama.” Hassan alisema baada ya kuikabidhi hospitali hiyo shehena ya vifaa mbali mbali aina ya PPE

Kadhalika Hassan aliahidi kuwa benki hiyo iko tayari kutoa ufadhili kama huo wakati wowote itakapohitajika.

 “Tulianza kuwapa msaada hospitali za kidini miezi tatu iliyopita na Hospitali ya Wamba, Maua, Meru, Nkubu. Iwapo kuna hospitali yoyote ya kidini inayohitaji msaada wa vifaa vya kujikinga nawaomba watembelee afisi zetu.”

Aidha ni ufadhili ambao umenufaisha hospitali kadhaa katika kaunti ya Isiolo huku wakitoa wito kwa hospitali za kidini kushirikiana na benki hiyo ili kuhakikisha wanainua hali ya huduma haswa kwa ufadhili wa vifaa muhimu.

 “Tunashukuru benki ya Equity kwa kutusaidia na vifaa hivi na tunatarajia kuanza kuwachanja na kupima wananchi virusi vya corona hivi karibuni.” Sr. Mercy Githinji ambaye ni msimamizi wa hospitali hiyo alisema wakati akivipokea vifaa hivyo rasmi.

RELATED ARTICLES

Ubomozi Mwangaza- usafiri watatizwa huku Magari yakichomwa na wakaazi kukesha usiku nje

Barabara kuu ya Isiolo kuelekea Meru, imefungwa kwa mda, hii ni baada ya wakaazi wenye ghadhabu wa eneo la mwangaza, kuifunga.

MWAKILISHI WA BABA MTAKATIFU AZURU JIMBO LA ISIOLO

By: Henry Mwangangi and Felix Mulei Mwakilishi wa baba mtakatifu nchini Kenya Askofu mkuu Hurbatus Van Megen Ijumaa alizuru...

Mwanaume ashtakiwa kwa kusafirisha bangi Isiolo.

By Jackline Mung’athia, 21st April 2021 Mwanaume wa umri wa makamo amefikishwa kwenye mahakama ya Isiolo Jumatano na kushtakiwa...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

MAAFISA WA EACC WAANZISHA RASMI MIKUTANO NA SEKTA MBALI MBALI ZA SERIKALI KATIKA KAUNTI YA ISIOLO

Mamlaka ya kupambana na ufisadi EACC, jumatatu  ilizindua rasmi mikutano katika  kanda ya  juu mashariki mwa nchi, na sekta mbalimbali...

“KUTI MUST GO!!!” A failed government or attention seeking?

As you take a walk around Isiolo town, for the past few months- you will see writings captioned "KUTI MUST GO!!!" On...

Wakaazi wa bullapesa walalamikia maendeleo duni, huku mwakilishi wao wa wadi akikosa kuhudhuria kikao

Wakaazi wa Bullapesa katika kaunti ya Isiolo wamelalamikia maendeleo duni katika wadi hiyo. Wakiongozwa na viongozi wa kamati ya kupanga maendeleo ya...

MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YATOA HUDUMA ZA AFYA BILA MALIPO KWA WAKAZI WA ISIOLO

Story By: Kelvin Mwingirwa Wakaazi wa eneo la bulapesa katika kaunti ya Isiolo Alhamisi walipokea huduma za matibabu ya...