Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Local News Viongozi walio na mazoea ya kuvuruga mikutano isiolo wazidi kushtumiwa

Viongozi walio na mazoea ya kuvuruga mikutano isiolo wazidi kushtumiwa

Kauli za kushtumu kisa ambacho kilitokea katika kaunti ya  Isiolo wakati wa ziara ya kinara wa odm raila, zimeendelea kutolewa wakati huu kisa hicho kikikashifiwa na waziri wa jinsia na maswala ya vijana Prof Margaret Kobia wakati wa ziara yake mjini Isiolo.

Akihutubu wakati wa hafla moja mjini Isiolo waziri kobia aliwataka wananchi kuwachagua viongozi walio na nia ya kuunganisha wakaazi kaunti ya Isiolo.

Mkichagua viongozi waadilifu wataleta maendeleo na kudumisha amani katika kaunti hii.” Kobia alisema

Kauli yake waziri Kobia iliungwa mkono na katibu mwandamizi wa wizara ya elimu nchini Mumina Bonaya ambaye alikashifu viongozi ambao walikuwa na tabia ya kupanga vurugu.

“Viongozi walio na tabia ya kupanga vurugu hawapaswi kuchaguliwa kwa sababu kila mtu ana uhuru wa kuuza sera zake mahali popote nchini.” Mumina alisema

Wakati uo huu Profesa kobia alimpongeza Mumina kwa kazi nzuri anayofanya kwenye sekta ya elimu kwani kaunti ya Isiolo inaongoza katika kanda ya kaskazini mashariki mwa nchi. “Kaunti ya Isiolo inaongoza katika kanda ya mashariki mwa nchi kuhakikisha wanazingatia wanafunzi wote wanajiunga na shule ya upili kazi nzuri Mumina.” Kobia alisema

Na huku usajili wa wapiga ukiendelea kote nchini waziri kobia alitoa wito kwa wakaazi isiolo kusajilishwa kama wapiga kura ili kuwachagua viongozi wafaao mwaka ujao.

“Tafadhali wananchi mjisajili kama wapiga kura ili muwachague viongozi wanaostahili.” Kobia alisema.

RELATED ARTICLES

MAAFISA WA EACC WAANZISHA RASMI MIKUTANO NA SEKTA MBALI MBALI ZA SERIKALI KATIKA KAUNTI YA ISIOLO

Mamlaka ya kupambana na ufisadi EACC, jumatatu  ilizindua rasmi mikutano katika  kanda ya  juu mashariki mwa nchi, na sekta mbalimbali...

“KUTI MUST GO!!!” A failed government or attention seeking?

As you take a walk around Isiolo town, for the past few months- you will see writings captioned "KUTI MUST GO!!!" On...

Wakaazi wa bullapesa walalamikia maendeleo duni, huku mwakilishi wao wa wadi akikosa kuhudhuria kikao

Wakaazi wa Bullapesa katika kaunti ya Isiolo wamelalamikia maendeleo duni katika wadi hiyo. Wakiongozwa na viongozi wa kamati ya kupanga maendeleo ya...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

MAAFISA WA EACC WAANZISHA RASMI MIKUTANO NA SEKTA MBALI MBALI ZA SERIKALI KATIKA KAUNTI YA ISIOLO

Mamlaka ya kupambana na ufisadi EACC, jumatatu  ilizindua rasmi mikutano katika  kanda ya  juu mashariki mwa nchi, na sekta mbalimbali...

“KUTI MUST GO!!!” A failed government or attention seeking?

As you take a walk around Isiolo town, for the past few months- you will see writings captioned "KUTI MUST GO!!!" On...

Wakaazi wa bullapesa walalamikia maendeleo duni, huku mwakilishi wao wa wadi akikosa kuhudhuria kikao

Wakaazi wa Bullapesa katika kaunti ya Isiolo wamelalamikia maendeleo duni katika wadi hiyo. Wakiongozwa na viongozi wa kamati ya kupanga maendeleo ya...

MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YATOA HUDUMA ZA AFYA BILA MALIPO KWA WAKAZI WA ISIOLO

Story By: Kelvin Mwingirwa Wakaazi wa eneo la bulapesa katika kaunti ya Isiolo Alhamisi walipokea huduma za matibabu ya...