Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Local News Wawaniaji wa uongozi Isiolo wahimizwa kushirikiana na kumteua kiongozi mmoja.

Wawaniaji wa uongozi Isiolo wahimizwa kushirikiana na kumteua kiongozi mmoja.

Wito umetolewa kwa wananchi kujitokeza kwa wingi na kujisajili kwani kura ni muhimu. Haya yanajiri huku mchakato wa usajili wa wapiga kura ukufikia mwisho.

Akizungumza kwenye hafla ya kuungwa mkono na wazee wa jamii ya Meru anayekimezea kiti cha ugavana wa kaunti ya Isiolo Hudson Kinyua, aliwahimiza wakaazi kujisajili ili kumchagua kiongozi atakayeleta maendeleo na kuwajali wananchi wote bila ubaguzi.

“Ninawaomba watu wajisajili kama wapiga kura kwani itakapowadia wakati wa kupiga kura utamchagua kiongozi ambaye hana ubaguzi.” Kinyua alisema

Wakati uo huo Kinyua aliwaomba viongozi wanaosimama nyadhifa  mbalimbali kutoka jamii moja kushirikiana na kuchagua kiongozi mmoja anayestahili.

“Hatutaruhusu kuwa na zaidi ya mwakilishi wadi mmoja katika wadi ya wabera na bula pesa kwa sababu hatutakubali ubinafsi wetu ifanye jamii ziendelee kuhangaika kwa miaka mingine tano, tutakaa na wazee na viongozi tukubaliane kiongozi mmoja atakayetuwakilisha.” Kinyua alisema

Wakati uo huo mwenyekiti wa muungano wa Ameru Turiamwe Paul Mugambi alidokeza kuwa wakaazi wamechoka kuwachagua viongozi ambao wanawatelekeza na kusisitiza kuwa watamuunga mkono Kinyua kwani wanaamini kuwa atashughulikia matakwa ya wakaazi wote katika kaunti ya Isiolo bila ubaguzi.

RELATED ARTICLES

MAAFISA WA EACC WAANZISHA RASMI MIKUTANO NA SEKTA MBALI MBALI ZA SERIKALI KATIKA KAUNTI YA ISIOLO

Mamlaka ya kupambana na ufisadi EACC, jumatatu  ilizindua rasmi mikutano katika  kanda ya  juu mashariki mwa nchi, na sekta mbalimbali...

“KUTI MUST GO!!!” A failed government or attention seeking?

As you take a walk around Isiolo town, for the past few months- you will see writings captioned "KUTI MUST GO!!!" On...

Wakaazi wa bullapesa walalamikia maendeleo duni, huku mwakilishi wao wa wadi akikosa kuhudhuria kikao

Wakaazi wa Bullapesa katika kaunti ya Isiolo wamelalamikia maendeleo duni katika wadi hiyo. Wakiongozwa na viongozi wa kamati ya kupanga maendeleo ya...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

MAAFISA WA EACC WAANZISHA RASMI MIKUTANO NA SEKTA MBALI MBALI ZA SERIKALI KATIKA KAUNTI YA ISIOLO

Mamlaka ya kupambana na ufisadi EACC, jumatatu  ilizindua rasmi mikutano katika  kanda ya  juu mashariki mwa nchi, na sekta mbalimbali...

“KUTI MUST GO!!!” A failed government or attention seeking?

As you take a walk around Isiolo town, for the past few months- you will see writings captioned "KUTI MUST GO!!!" On...

Wakaazi wa bullapesa walalamikia maendeleo duni, huku mwakilishi wao wa wadi akikosa kuhudhuria kikao

Wakaazi wa Bullapesa katika kaunti ya Isiolo wamelalamikia maendeleo duni katika wadi hiyo. Wakiongozwa na viongozi wa kamati ya kupanga maendeleo ya...

MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YATOA HUDUMA ZA AFYA BILA MALIPO KWA WAKAZI WA ISIOLO

Story By: Kelvin Mwingirwa Wakaazi wa eneo la bulapesa katika kaunti ya Isiolo Alhamisi walipokea huduma za matibabu ya...