Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News National News SIKU YA KIMATAIFA KUKOMESHA DHULUMA DHIDI YA WANAHABARI YAADHIMISHWA

SIKU YA KIMATAIFA KUKOMESHA DHULUMA DHIDI YA WANAHABARI YAADHIMISHWA

Mkurugenzi wa mashtaka ya uma DPP Noordin Haji jumanne aliwahakikishia wanahabari kwamba watalindwa vya kutosha dhidi ya vitisho wanapotekeleza kazi yao. Wakati uohuo, Haji aliwataka waandishi wa habari kutekeleza kazi yao kwa kuzingatia usawa ili kuepuka uchochezi kwa misingi ya kikabila.

Aliyasema haya wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kukomesha dhuluma dhidi ya waandishi wa habari.

“Japo kuna vitisho vya aina mbalimbali dhidi ya wanahabari, nawahimiza wasikome kuuliza maswali nyeti yanayoangazia changamoto tunazopitia kama nchi na vilevile ukiukaji wa sheria nchini,” Haji akasema

Siku hii huadhimishwa tarehe mbili November, ili kutoa hamasisho kuhusu haki ya uandishi wa habari na vilevile kupigana na uhalifu dhidi ya wanahabari.

Baraza la wanahabari nchini Kenya liliadhimisha siku hii kwa ushirikiano na shirika la umoja wa mataifa kuhusu elimu, sayanzi na utamaduni UNESCO.

Mkurugenzi wa UNESCO eneo la Africa mashariki Profesa Hubert Gijzen alisema kuwa waandishi wa habari wanapitia changamoto tele za vitisho, kushambuliwa na unyanyasaji hasa kwenye mitandao.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa MCK Maina Muiruri alilalamika kuwa ukosefu wa uchunguzi kwenye kesi zinazohusu dhuluma dhidi ya wanahabari umeadhiri usalama wao.

“Visa vya dhuluma dhidi ya waandishi wa habari vimeongezeka sana tangu miaka mitatu iliyopita…vitengo vya usalama ndivyo vinavyoongoza kwenye idadi ya vitisho dhidi ya wanahabari,” Mwenyekiti wa MCK alisema.

Aidha alidokeza kwamba wanaotekeleza uhalifu huo wamekosa kufunguliwa mashtaka.

RELATED ARTICLES

POLISI WATALINDA WANAHABARI WAKATI WA UCHAGUZI, ASEMA INSPEKTA MKUU

Idara ya polisi itajizatiti kuhakikisha usalama kwa waandishi wa habari nchini, hasa wakati huu taifa linapoelekea kwenye uchaguzi mkuu mwakani. Hii ndiyo...

TRUE, Poultry farming supports over 160 households in Uasin Gishu County

A Facebook post claiming that poultry farming supports over 160 households in Uasin Gishu county is true based on a study conducted...

RAIS KENYATTA AANDAA MKUTANO BAINA YA RAILA NA VINARA WA ONE KENYA

Rais Uhuru Kenyatta leo amekutana na viongozi watano wa vyama vya kisiasa humu nchini. Ni mkutano ambao umekisiwa wa kujaribu kuwaunganisha Raila...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

MAAFISA WA EACC WAANZISHA RASMI MIKUTANO NA SEKTA MBALI MBALI ZA SERIKALI KATIKA KAUNTI YA ISIOLO

Mamlaka ya kupambana na ufisadi EACC, jumatatu  ilizindua rasmi mikutano katika  kanda ya  juu mashariki mwa nchi, na sekta mbalimbali...

“KUTI MUST GO!!!” A failed government or attention seeking?

As you take a walk around Isiolo town, for the past few months- you will see writings captioned "KUTI MUST GO!!!" On...

Wakaazi wa bullapesa walalamikia maendeleo duni, huku mwakilishi wao wa wadi akikosa kuhudhuria kikao

Wakaazi wa Bullapesa katika kaunti ya Isiolo wamelalamikia maendeleo duni katika wadi hiyo. Wakiongozwa na viongozi wa kamati ya kupanga maendeleo ya...

MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YATOA HUDUMA ZA AFYA BILA MALIPO KWA WAKAZI WA ISIOLO

Story By: Kelvin Mwingirwa Wakaazi wa eneo la bulapesa katika kaunti ya Isiolo Alhamisi walipokea huduma za matibabu ya...