Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News National News POLISI WATALINDA WANAHABARI WAKATI WA UCHAGUZI, ASEMA INSPEKTA MKUU

POLISI WATALINDA WANAHABARI WAKATI WA UCHAGUZI, ASEMA INSPEKTA MKUU

Idara ya polisi itajizatiti kuhakikisha usalama kwa waandishi wa habari nchini, hasa wakati huu taifa linapoelekea kwenye uchaguzi mkuu mwakani. Hii ndiyo kauli ya Inspekta mkuu wa Polisi nchini Kenya Hillary Mutyambai.

Akiongea wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa kukomesha dhuluma dhidi ya wanahabari, Inspekta mkuu alisema kwamba idara yake ingeendelea kuhusisha vyombo vya habari na washikadau wengine katika kuleta uwajibikaji kwenye idara ya polisi.

Kwenye taarifa iliyosomwa na msaidizi wake mkuu Munga Nyale , Mutyambai alisema kuwa polisi itawahakikishia wanahabari uhuru wa kufanya kazi yao pasipo mwingilio wowote. Vile vile alionyesha umuhimu wa ushirikiano kati ya idara hizo mbili.

“Ipo haja ya kuboresha uhusiano baina ya idara ya usalama na idara ya wanahabari ili kulishughulikia changamoto zinazotokana na vitisho dhidi ya waandishi wa habari,” Mutyambai alihimiza.

Kufikia mwezi October mwaka huu, visa 55 vya wanahabari kudhulumiwa vimeripotiwa. Hii ni Kulingana na baraza la wanahabari la Kenya MCK.

Hata hivyo, Mutyambai alihimiza kwamba idara ya habari na idara ya polisi zina jukumu kuu kwenye la kuhakikisha haki wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.

RELATED ARTICLES

SIKU YA KIMATAIFA KUKOMESHA DHULUMA DHIDI YA WANAHABARI YAADHIMISHWA

Mkurugenzi wa mashtaka ya uma DPP Noordin Haji jumanne aliwahakikishia wanahabari kwamba watalindwa vya kutosha dhidi ya vitisho...

TRUE, Poultry farming supports over 160 households in Uasin Gishu County

A Facebook post claiming that poultry farming supports over 160 households in Uasin Gishu county is true based on a study conducted...

RAIS KENYATTA AANDAA MKUTANO BAINA YA RAILA NA VINARA WA ONE KENYA

Rais Uhuru Kenyatta leo amekutana na viongozi watano wa vyama vya kisiasa humu nchini. Ni mkutano ambao umekisiwa wa kujaribu kuwaunganisha Raila...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

MAAFISA WA EACC WAANZISHA RASMI MIKUTANO NA SEKTA MBALI MBALI ZA SERIKALI KATIKA KAUNTI YA ISIOLO

Mamlaka ya kupambana na ufisadi EACC, jumatatu  ilizindua rasmi mikutano katika  kanda ya  juu mashariki mwa nchi, na sekta mbalimbali...

“KUTI MUST GO!!!” A failed government or attention seeking?

As you take a walk around Isiolo town, for the past few months- you will see writings captioned "KUTI MUST GO!!!" On...

Wakaazi wa bullapesa walalamikia maendeleo duni, huku mwakilishi wao wa wadi akikosa kuhudhuria kikao

Wakaazi wa Bullapesa katika kaunti ya Isiolo wamelalamikia maendeleo duni katika wadi hiyo. Wakiongozwa na viongozi wa kamati ya kupanga maendeleo ya...

MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YATOA HUDUMA ZA AFYA BILA MALIPO KWA WAKAZI WA ISIOLO

Story By: Kelvin Mwingirwa Wakaazi wa eneo la bulapesa katika kaunti ya Isiolo Alhamisi walipokea huduma za matibabu ya...