Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Local News Viongozi wa vijana wafanya kikao Isiolo kujadili maswala ya kujiinua kabla ya...

Viongozi wa vijana wafanya kikao Isiolo kujadili maswala ya kujiinua kabla ya Uchaguzi.

Viongozi wa vijana kutoka kaunti ya TharakaNithi, Meru, Marsabit na Isiolo walikongamana katika kanisa moja katika kaunti ya Isiolo kwa madhumuni ya kujadiliana jinsi watakavyosonga mbele na kujiinua,  kama njia ya kujimudu maisha ya usoni.

Walipokuwa wakizungumza na wanahabari, vijana hao walidokeza kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakitelekezwa na huu ndio wakati wa kusimama na kutetea haki zao.

“Tumeungana kama wanarika kutoka kaunti nne kwa sababu tunataka sauti yetu isikike na ni lazima maslahi yetu yashughulikiwe.” vijana walisema

Vijana hao aidha, walitoa wito kwa vijana wenzao kuwania nyadhifa mbalimbali za uongozi ili wahusishwe katika uamuzi wa maendeleo ya nchi.

“Sisi tuko tayari kuwaunga mkono vijana wenzetu watakaosimama kuwania nyadhifa za uongozi na tumekubaliana kuwa hatutatumiwa vibaya na wanasiasa kuleta vurugu”

Mwakilishi wa vijana wa muungano wa makanisa nchini NCCK katika kanda la mashariki Rev Linda Mwirigi alisisitiza kuwa vijana wanao uwezo, ila wanatelekezwa.

“Tumegundua kuwa tumekuwa tukitelekezwa ingawaje tuna uwezo na tumeamua kuingia uongozini ili tuhusishwe katika uamuzi.” Linda alisema 

Wakati uo huo vijana hao walisema kuwa wanatafuta njia za kupambana na changamoto ya ukosefu wa ajira na kuomba usaidizi kwa serikali kukuza talanta za vijana.

“Tunaomba serikali kusaidia kwenye ukuzaji wa talanta za vijana na kutuunga mkono katika shughuli zinazotuletea ajira ili tujiinue kiuchumi na kujiepusha kutokana na maadili potovu.” Vijana walisema

RELATED ARTICLES

MAAFISA WA EACC WAANZISHA RASMI MIKUTANO NA SEKTA MBALI MBALI ZA SERIKALI KATIKA KAUNTI YA ISIOLO

Mamlaka ya kupambana na ufisadi EACC, jumatatu  ilizindua rasmi mikutano katika  kanda ya  juu mashariki mwa nchi, na sekta mbalimbali...

“KUTI MUST GO!!!” A failed government or attention seeking?

As you take a walk around Isiolo town, for the past few months- you will see writings captioned "KUTI MUST GO!!!" On...

Wakaazi wa bullapesa walalamikia maendeleo duni, huku mwakilishi wao wa wadi akikosa kuhudhuria kikao

Wakaazi wa Bullapesa katika kaunti ya Isiolo wamelalamikia maendeleo duni katika wadi hiyo. Wakiongozwa na viongozi wa kamati ya kupanga maendeleo ya...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

MAAFISA WA EACC WAANZISHA RASMI MIKUTANO NA SEKTA MBALI MBALI ZA SERIKALI KATIKA KAUNTI YA ISIOLO

Mamlaka ya kupambana na ufisadi EACC, jumatatu  ilizindua rasmi mikutano katika  kanda ya  juu mashariki mwa nchi, na sekta mbalimbali...

“KUTI MUST GO!!!” A failed government or attention seeking?

As you take a walk around Isiolo town, for the past few months- you will see writings captioned "KUTI MUST GO!!!" On...

Wakaazi wa bullapesa walalamikia maendeleo duni, huku mwakilishi wao wa wadi akikosa kuhudhuria kikao

Wakaazi wa Bullapesa katika kaunti ya Isiolo wamelalamikia maendeleo duni katika wadi hiyo. Wakiongozwa na viongozi wa kamati ya kupanga maendeleo ya...

MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YATOA HUDUMA ZA AFYA BILA MALIPO KWA WAKAZI WA ISIOLO

Story By: Kelvin Mwingirwa Wakaazi wa eneo la bulapesa katika kaunti ya Isiolo Alhamisi walipokea huduma za matibabu ya...