Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Local News Wakaazi wa bullapesa walalamikia maendeleo duni, huku mwakilishi wao wa wadi akikosa...

Wakaazi wa bullapesa walalamikia maendeleo duni, huku mwakilishi wao wa wadi akikosa kuhudhuria kikao

Wakaazi wa Bullapesa katika kaunti ya Isiolo wamelalamikia maendeleo duni katika wadi hiyo. Wakiongozwa na viongozi wa kamati ya kupanga maendeleo ya wadi WPC, walisema kuwa wadi hiyo imesalia nyuma kimaendeleo ikilinganishwa na fedha zinazotengewa maendeleo kwa wadi hiyo. Waliyasema  hayo walipokuwa wakilikabidhi bunge la kaunti mahitaji yanayohitaji kupewa kipaumbele katika mpango wa miradi ya mwaka wa fedha 2021/22.

Miradi waliyotaka ishughulikiwe kwanza ni ile ya; kupanuliwa kwa kituo cha afya cha Bullapesa, kutengezwa kwa barabara na kusajiliwa kwa ardhi.

“Kupitia kupanuliwa kwa baadhi ya barabara, ni vyema pia kushughulikia barabara ndogo zinazoongoza kwa barabara kuu, kwa sababu bila hizo barabara hatuwezi tukaenda katika vituo vya afya. Kwa hivyo wakati huu wa mvua, barabara za bullapesa, ni mbovu kabisa- na tunaomba serikali izishughulikie” Walisema wanakamati wa WPC.

Aidha, wakaazi hao walishutumu serikali ya kaunti, kwa kutengea miradi fedha- ila miradi hiyo haitekelezwi. Vile vile, kufuatia kupitishwa kwa sera ya kupambana na mchafuko wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi, wali-itaka serikali kuhakikisha kuwa asilimia mbili ya bajeti ya kaunti inayotengewa shugli hiyo, inapitia kwa kamati za wadi ili kuhakikisha kuwa swala hilo linatatuliwa.

Hivi vitu vimetengewa pesa katika bajeti. Lakini ukifika wakati wakufanya miradi hiyo, hatuioni. Sasa umefika wakati ambapo tunayotaka kuona ni kazi ikitendeka.” Alisema Lydia Ntinyari, katibu wa WPC wadi ya Bullapesa

Apo awali, pesa hizo  katika bajeti ya kaunti, zilikuwa zikitumika katika sekta nyinginezo kwa kukosekana kamati ya kuunda miradi itakayoshughulikia maswala ya mabadiliko ya tabia nchi na mchafuko wa mazingira kati viwango vya wadi.

WPC na wakaazi wakiyakabidhi matakwa yao kwa bunge la kaunti.

Aliyeyapokea matakwa hayo kutoka kwa wananchi, ni mwakilishi wa wadi ya Wabera Mwalimu Abdi Duba, huku mwakilishi wa wadi ya Bullapesa Idd-Hassan Kimathi akikosa kuhudhuria mkutano huo.

 Katika hafla iliyofanyika wiki mbili zilizopita, ya kumuunga mkono Kinyua Shalom kuwania kiti cha ugavana, Idd Kim, aliwataka wananchi wa Bullapesa kumuwia radhi kwa kukosa kuwa nao kwa miaka minne, na kuwataka wamchague tena katika uchaguzi ujao.

RELATED ARTICLES

MAAFISA WA EACC WAANZISHA RASMI MIKUTANO NA SEKTA MBALI MBALI ZA SERIKALI KATIKA KAUNTI YA ISIOLO

Mamlaka ya kupambana na ufisadi EACC, jumatatu  ilizindua rasmi mikutano katika  kanda ya  juu mashariki mwa nchi, na sekta mbalimbali...

“KUTI MUST GO!!!” A failed government or attention seeking?

As you take a walk around Isiolo town, for the past few months- you will see writings captioned "KUTI MUST GO!!!" On...

MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YATOA HUDUMA ZA AFYA BILA MALIPO KWA WAKAZI WA ISIOLO

Story By: Kelvin Mwingirwa Wakaazi wa eneo la bulapesa katika kaunti ya Isiolo Alhamisi walipokea huduma za matibabu ya...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

MAAFISA WA EACC WAANZISHA RASMI MIKUTANO NA SEKTA MBALI MBALI ZA SERIKALI KATIKA KAUNTI YA ISIOLO

Mamlaka ya kupambana na ufisadi EACC, jumatatu  ilizindua rasmi mikutano katika  kanda ya  juu mashariki mwa nchi, na sekta mbalimbali...

“KUTI MUST GO!!!” A failed government or attention seeking?

As you take a walk around Isiolo town, for the past few months- you will see writings captioned "KUTI MUST GO!!!" On...

Wakaazi wa bullapesa walalamikia maendeleo duni, huku mwakilishi wao wa wadi akikosa kuhudhuria kikao

Wakaazi wa Bullapesa katika kaunti ya Isiolo wamelalamikia maendeleo duni katika wadi hiyo. Wakiongozwa na viongozi wa kamati ya kupanga maendeleo ya...