Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Local News MAAFISA WA EACC WAANZISHA RASMI MIKUTANO NA SEKTA MBALI MBALI ZA SERIKALI...

MAAFISA WA EACC WAANZISHA RASMI MIKUTANO NA SEKTA MBALI MBALI ZA SERIKALI KATIKA KAUNTI YA ISIOLO

Mamlaka ya kupambana na ufisadi EACC, jumatatu  ilizindua rasmi mikutano katika  kanda ya  juu mashariki mwa nchi, na sekta mbalimbali za  serikali katika kaunti ya Isiolo, ili kuwahamasisha maafisa wa serikali kuhusiana na hadhari na jinsi ya kuzuia ufisadi.

Katika hotuba yake, msimamizi wa kanda hiyo, bwana George Ojowi- alisisitiza umuhimu wa kuwahusisha wananchi kwa uwazi hili kupelekea kupunguka kwa visa vya ufisadi nchini. Aidha, aliwaeleza wananchi umuhimu wa kujizuia kutokana na visa vya ufisadi ili kuleta maendeleo  katika kaunti kwa kuzuia utumizi mbaya wa mali ya umma.

“tutakuwa na mafunzo na kuhamasisha, katika sekta zote za serikali kaunti hii, bunge, waandishi wa habari na pia tutakuja ‘mashinani’ kwa wananchi hili kupata kujua maswala ambayo mngependa yaangaziwe,” alisema Ojowi.

Gavana Kuti katika hafla iliyohudhuriwa na maafisa kutoka afisi za Mamlaka ya EACC

Kwa upande wake gavana wa kaunti ya Isiolo  Dkt Mohamed Kuti alisema kuwa kama serikali ya kaunti imejaribu kila iwezalo kurekebisha mianya inayopelekea kupotea,  ama kutumiwa vibaya kwa raslimali ya umma, na kusema  kuwa serikali ya kaunti imefaulu katika kuzuia uvujaji wa fedha, akiyataja  maendeleo kadha aliyosema  kuonekana mjini kama ushahidi wa kuonyesha kwamba pesa za umma zinatumika ipasavyo.

“Tumewahakikishia (maafisa wa EACC) kwamba tutashirikiana nao katika serikali na bunge la kaunti ya Isiolo, pale mumeona kuna upungufu tutakuwa tayari pia kurekebisha,” alisema gavana Kuti.

Maafisa wa serikali ya kaunti ya Isiolo na wananchi katika hafla ya kuzindua uhamasishaji kuhusiana na ufisadi katika kaunti ya Isiolo

Haya yanajiri huku taifa na ulimwengu mzima ukizidi kujitayarisha kuadhimisha siku ya kupigana na ufisadi duniani, sherehe ambazo ufanyika kila tarehe tisa mwezi wa desemba, sherehe kuu za mwaka huu zikipaniwa kufanyika kaunti ya Mombasa, nazo zile za kanda ya juu mashariki, inayohusisha kaunti za Isiolo, Samburu, Marsabit, Meru na Tharaka Nithi zikiadhimishwa katika kaunti ya Isiolo.

RELATED ARTICLES

“KUTI MUST GO!!!” A failed government or attention seeking?

As you take a walk around Isiolo town, for the past few months- you will see writings captioned "KUTI MUST GO!!!" On...

Wakaazi wa bullapesa walalamikia maendeleo duni, huku mwakilishi wao wa wadi akikosa kuhudhuria kikao

Wakaazi wa Bullapesa katika kaunti ya Isiolo wamelalamikia maendeleo duni katika wadi hiyo. Wakiongozwa na viongozi wa kamati ya kupanga maendeleo ya...

MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YATOA HUDUMA ZA AFYA BILA MALIPO KWA WAKAZI WA ISIOLO

Story By: Kelvin Mwingirwa Wakaazi wa eneo la bulapesa katika kaunti ya Isiolo Alhamisi walipokea huduma za matibabu ya...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

MAAFISA WA EACC WAANZISHA RASMI MIKUTANO NA SEKTA MBALI MBALI ZA SERIKALI KATIKA KAUNTI YA ISIOLO

Mamlaka ya kupambana na ufisadi EACC, jumatatu  ilizindua rasmi mikutano katika  kanda ya  juu mashariki mwa nchi, na sekta mbalimbali...