Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Church News KANISA KATOLIKI ISIOLO LAWAFAA WATU WENYE CHANGAMOTO ZA MAUMBILE

KANISA KATOLIKI ISIOLO LAWAFAA WATU WENYE CHANGAMOTO ZA MAUMBILE

KELVIN MWINGIRWA

Mamia ya wa wakaazi wanaoishi na changamoto za ki maumbile katika eneo la kandebene iliyopo katika mpaka wa isiolo na meru, jumapili walipokea msaada wa chakula kutoka kwa wahisani.

Kwenye hafla iliyoandaliwa na kanisa katoliki parokia ya St. Eusebius hapa Isiolo, wahisani mbalimbali walijitokeza kutoa bidhaa kama vile chakula na nguo.

Hafla iyo huandaliwa mara moja kila mwaka na chama cha wanaume wakatoliki (CMA) kutoka parokia ya mtakatifu Eusebius, kwa madhumuni ya kuwaleta watu wote wenye changamoto za kimaumbele pamoja na pia kuwaleta wahisani kutoka nyadhifa mbali mbali katika kaunti ya isiolo ili kuwapa usaidizi na pia kuzungumzia changamoto zinazowakumba.

Mwaniaji wa kiti cha ubunge cha isiolo kaskazini Mwenda Thuranira ambaye alikuwa mmoja wa wahisani wakuu kwenye hafla hiyo iliyoandaliwa katika kanisa katoliki la kandebene, amesema watu wanaoishi na ulemavu mara nyingi wanatelekezwa na katika jamii na hata katika nyadhifa za uongozi.

Vilevile amewarai wazazi ambao wakona watoto wanaoishi na changamoto za kimaumbile waache kuwaficha au kuwabagua.

“Hakuna mswada hata mmoja uliobuniwa bungeni kwa miaka kumi sasa kutoka kwa mbunge yeyote kutoka Isiolo kaskazini kuhusu watu wenye ulemavu. Hawa watu wanachaguliwa wa nini kama hawatawakilisha wakazi wao?” alisema Bw Thuranira.

Thuranira aliweza kutoa viti 74 vyenye magurudumu kwa watu wanaoishi na ulemavu wakati wa hafla hiyo, huku akiahidi kutoa nyingine Zaidi kabla mwisho wa mwaka 2021.

Kenya ilijiunga na ulimwengu mzima kuadhimisha siku ya watu walio na changamoto za kimaumbile tarehe 3rd December 2021 katika ukumbi wa mikutano wa KICC, ambapo waziri Margaret Kobia alisema watu wanaoishi na changamoto za ulemavu wanaweza kuchangia zaidi katika maendeleo ya nchi wakipatiwa nafasi za uongozi.

RELATED ARTICLES

WAKENYA WANA HAKI YA KUMCHAGUA KIONGOZI WANAYEMTAKA, ASKOFU IRERI ASEMA

Askofu wa jimbo katoliki la Isiolo Anthony Ireri Mukobo amewarai wananchi kufanya maamuzi mwafaka kuhusu viongozi kwa kutathmin sera na wala si...

MONSIGNOR KADIMA, ATEULIWA KAMA ASKOFU MPYA WA BUNGOMA

Baba mtakatifu papa Francis Jumanne tarehe 14 December, 2021 alimteua padre Monsignor Mark Kadima kuwa askofu wa jimbo katoliki la Bungoma. Taarifa...

Pope Francis appoints Archbishop Philip Anyolo as Archbishop of Nairobi

The Holy Father Pope Francis has appointed the Archbishop of the Catholic Archdiocese of Kisumu, Most Rev. Philip A. Anyolo, as Archbishop...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

St. Emilie de Vialar

18th January St. Emilie de Vialar (Emily) was born in 1797 in Gaillac and ancient town in the south...

Readings at Mass Tuesday 18 January 2022

Second Week in Ordinary Time  Liturgical Colour: Green. First reading 1 Samuel 16:1-13

WENYEKITI WA BODABODA ISIOLO KUSHIRIKIANA NA VITENGO VYA USALAMA ILI KUPELEKEA KUMALIZIKA KWA UHALIFU

Muungano wa wenyekiti wa wahudumu wa bodaboda Isiolo, umesema kushirikiana Pamoja na maafisa wa  kulinda usalama, ili kumaliza uhalifu katika kaunti hii....

Msako mkali wa pombe haramu wafanyika Isiolo.

Idara ya NGAO katika kaunti ya Isiolo wamefanya msako wa pombe haramu katika eneo la Bula Pesa katika kaunti hii.