Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Local News Vijana 32 kaunti ya Isiolo wabadilisha mienendo yao ya matumizi ya mihadarati.

Vijana 32 kaunti ya Isiolo wabadilisha mienendo yao ya matumizi ya mihadarati.

Vijana 40 katika kaunti ya Isiolo wameungana na kuunda kikundi kiitwacho “Tupendane” kwa lengo la kusaidia wasiojiweza na kuwahamasisha vijana dhidi ya matumizi ya mihadarati.

Akizungumza na radio shahidi kwa njia ya kipekee, mwenyekiti wa kikundi hicho Miriam Mumbi, alisema kuwa kupitia hamasisho ambalo wamekuwa wakifanya kwa vijana wasio na makazi rasmi wamefanikiwa kuwabadili vijana wengi kuacha kutumia dawa za kulevya.

“Vijana 32 wasio na makazi rasmi wameacha matumizi ya mihadarati na wameapa kueneza hamasisho kwa vijana ili kuacha mihadarati.” Mumbi asema

Baadhi ya vijana ambao wamebadilika na kuacha kutumia mihadarati walishukuru kikundi hicho kwa kuwaelimisha kuhusiana na madhara ya dawa za kulevya na wakaapa kuwabadili wenzao ambao wangali wanatumia mihadarati. Vile vile walitoa wito kwa vijana wengineo wanaotumia mihadarati kuacha ili kuboresha maisha ya usoni, “Tunashukuru kikundi cha Tupendane kwa kutusaidia kuacha kutumia mihadarati. Naomba vijana wenzangu waache kutumia dawa za kulevya kwa sababu hazitawasaidia.”

Wakati uo huo vijana hao walitoa wito kwa serikali ya kaunti kuingilia kati na kuwasaidia kwa kuwapa kazi vijana waliobadilika ili wasirejelee uraibu wa mihadarati.

“Tunaomba serikali ya kaunti na mashirika yasiyo ya kiserikali kutusaidia kwa kujenga pahali pa kukaa na kufanya kazi ili watu walioacha kutumia mihadarati wasirejelee.” Mumbi asema

RELATED ARTICLES

WENYEKITI WA BODABODA ISIOLO KUSHIRIKIANA NA VITENGO VYA USALAMA ILI KUPELEKEA KUMALIZIKA KWA UHALIFU

Muungano wa wenyekiti wa wahudumu wa bodaboda Isiolo, umesema kushirikiana Pamoja na maafisa wa  kulinda usalama, ili kumaliza uhalifu katika kaunti hii....

Msako mkali wa pombe haramu wafanyika Isiolo.

Idara ya NGAO katika kaunti ya Isiolo wamefanya msako wa pombe haramu katika eneo la Bula Pesa katika kaunti hii.

ONYO DHIDI YA VIONGOZI WA JAMII WANAOTOA MATAMSHI YA UCHOCHEZI

Onyo kali limetolewa dhidi ya wanasiasa wanaotumia viongozi wa jamii kuchochea wananchi kwani watachukuliwa hatua kali za kisheria. Viongozi...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

St. Emilie de Vialar

18th January St. Emilie de Vialar (Emily) was born in 1797 in Gaillac and ancient town in the south...

Readings at Mass Tuesday 18 January 2022

Second Week in Ordinary Time  Liturgical Colour: Green. First reading 1 Samuel 16:1-13

WENYEKITI WA BODABODA ISIOLO KUSHIRIKIANA NA VITENGO VYA USALAMA ILI KUPELEKEA KUMALIZIKA KWA UHALIFU

Muungano wa wenyekiti wa wahudumu wa bodaboda Isiolo, umesema kushirikiana Pamoja na maafisa wa  kulinda usalama, ili kumaliza uhalifu katika kaunti hii....

Msako mkali wa pombe haramu wafanyika Isiolo.

Idara ya NGAO katika kaunti ya Isiolo wamefanya msako wa pombe haramu katika eneo la Bula Pesa katika kaunti hii.