Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Church News MONSIGNOR KADIMA, ATEULIWA KAMA ASKOFU MPYA WA BUNGOMA

MONSIGNOR KADIMA, ATEULIWA KAMA ASKOFU MPYA WA BUNGOMA

Baba mtakatifu papa Francis Jumanne tarehe 14 December, 2021 alimteua padre Monsignor Mark Kadima kuwa askofu wa jimbo katoliki la Bungoma. Taarifa ya kuteuliwa kwa Kadima ilichapishwa kwenye jarida la L’Osservatore Romano mjini Roma Italia Jumanne saa sita mchana majira ya Roma, sawa na saa nane adhuhuri majira ya Afrika mashariki 14 December, 2021.

Mwakilishi wa baba mtakatifu nchini Kenya na Sudan Kusini, askofu mkuu Hubertus Van Megen alituma pia taarifa rasmi ya uteuzi huu kwa baraza la maskofu wa katoliki KCCB. Kwenye barua hiyo ya kitume, askofu mkuu Van Megen aliandika, “nina furaha kuwaarifu kwamba Papa Francis amemteua padre Monsignor Mark Kadima kama askofu wa Bungoma.”

Askofu mteule Kadima atarithi nafasi iliyowachwa na askofu Norman King’oo ambaye alihamishwa kwenda kuhudumu katika jimbo katoliki la Machakos. Tangu uhamisho huo, askofu wa jimbo katoliki la Kakamega Joseph Obanyi Sagwe alikuwa akihudumu kama msimamizi wa jimbo la Bungoma.

Askofu mteule Kadima alizaliwa mnamo tarehe 30 Aprili 1964 katika eneo la Kholera, kaunti ya Kakamega na kupokea daraja la upadrisho katika jimbo katoliki la Kakamega tarehe 2 October, 1993.

Kadima alihudhuria shule ya msingi ya Kholera kati ya mwaka 1972 na 1978, kisha akajiunga na St. Peter’s Seminary Mukumu, Kakamega 1979-1982, na Tindinyo College 1983-1984. Baadaye alijiunga na St. Mary’s Seminary Molo kwa majiundo ya kitume 1985, kabla ya kuingia St. Augustine’s Senior Seminary, Mabanga Bungoma kwa majiundo ya falsafa 1986 to 1987. Askofu mteule Kadima alijiunga na chuo cha Pontifical Urbanian University mjini Roma na kuhitimu shahada ya Philosophia (1987 – 1988), Theolojia (1988 – 1991), na Canon Law (1991 – 1993).

Baada ya upadrisho wake 1993, alihudumu katika parokia ya Shiseso kama padre msaidizi. Tarehe 16th Agosti, 1996, aliteuliwa kuwa msimamizi wa seminari ndogo ya St. Peter’s Mukumu. Alihudumu pia kwenye nyadhifa mbalimbali kama mshirikishi wa jimbo kwenye tume ya CJPC, Mshauri wa sheria ya kanisa kwenye jimbo, mwanachama wa bodi na chama cha sheria ya kanisa nchini Kenya CLSK, miongoni mwa nyingine.

Kabla ya uteuzi wake kama askofu wa Bungoma, Monsignor Kadima alikuwa akitumika kama msimamizi wa masuala ya kitume nchini Sudan Kusini.

RELATED ARTICLES

WAKENYA WANA HAKI YA KUMCHAGUA KIONGOZI WANAYEMTAKA, ASKOFU IRERI ASEMA

Askofu wa jimbo katoliki la Isiolo Anthony Ireri Mukobo amewarai wananchi kufanya maamuzi mwafaka kuhusu viongozi kwa kutathmin sera na wala si...

KANISA KATOLIKI ISIOLO LAWAFAA WATU WENYE CHANGAMOTO ZA MAUMBILE

KELVIN MWINGIRWA Mamia ya wa wakaazi wanaoishi na changamoto za ki maumbile katika eneo la kandebene iliyopo katika mpaka...

Pope Francis appoints Archbishop Philip Anyolo as Archbishop of Nairobi

The Holy Father Pope Francis has appointed the Archbishop of the Catholic Archdiocese of Kisumu, Most Rev. Philip A. Anyolo, as Archbishop...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

St. Emilie de Vialar

18th January St. Emilie de Vialar (Emily) was born in 1797 in Gaillac and ancient town in the south...

Readings at Mass Tuesday 18 January 2022

Second Week in Ordinary Time  Liturgical Colour: Green. First reading 1 Samuel 16:1-13

WENYEKITI WA BODABODA ISIOLO KUSHIRIKIANA NA VITENGO VYA USALAMA ILI KUPELEKEA KUMALIZIKA KWA UHALIFU

Muungano wa wenyekiti wa wahudumu wa bodaboda Isiolo, umesema kushirikiana Pamoja na maafisa wa  kulinda usalama, ili kumaliza uhalifu katika kaunti hii....

Msako mkali wa pombe haramu wafanyika Isiolo.

Idara ya NGAO katika kaunti ya Isiolo wamefanya msako wa pombe haramu katika eneo la Bula Pesa katika kaunti hii.