Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Features SERIKALI ISIYOJALI, AMA WATU KUKOSA MAKAAZI? ;JALALA HATARI-ISIOLO

SERIKALI ISIYOJALI, AMA WATU KUKOSA MAKAAZI? ;JALALA HATARI-ISIOLO

Jaa la takataka la Charko katika eneo la kambi garba kaunti ya Isiolo ni pahala ambapo binadamu hawezi tamani kuishi kutokana na uvundo wa maji taka, vyakula vilivyooza na takataka iliyotapakaa eneo hili.

Ng’ombe, mbuzi na baadhi ya ndege wa angani hupata lishe katika eneo hili. Licha ya taswira hiyo, baadhi ya familia zisizo na makaazi katika kaunti ya Isiolo zimepata hifadhi katika jalala hili.

Makumi ya watu pamoja na watoto wao kila siku hufika kwenye jaa hili kujitafutia riziki ya kila siku kwa kuokota takataka, vyuma na karatasi na kisha kuziuza. La kusikitisha ni kwamba zipo familia zenye watoto wachanga, wazee na kina mama zinazoishi hapa kwa kukosa makaazi rasmi.

Baadhi ya Familia zilizolifanya jalala hilo makaazi yao

“Tunategemea jaa hili kupata riziki ya kila siku, Sisi huamka asubuhi kuokota vyuma, karatasi na kuziuza na hivyo tunapata hela za kununua chakula.” Familia wasema.

Msimamizi wa manispaa ya kaunti ya Isiolo Halake Osman amesema kuwa eneo hilo linatumika kwa muda huku serikali ya kaunti ikiwa na mpango wa kujenga jaa kubwa kwingineko.

“Tuna mpango wa kutengeneza jaa lingine mbali na mji wa Isiolo na tumeajiri mlinzi anayelinda mchana tu kwa sababu eneo hilo watu huibiwa. Tumeweka ua la kulinda eneo hilo mara tatu ikiibiwa.” Osman asema

Pembezoni mwa jaa hili, ni vibanda vilivyojengwa kwa kutumia karatasi na takataka nyinginezo. Vibanda hivi ni nyumba za baadhi ya familia zinazotegemea jaa hili. Nyumba ambazo haziwezi kustahimili mvua au upepo mkali. Hata hivyo wanajikaza kutafuta lishe kwa watoto wao huku wakipishana na kunguru na mifugo wengineo.

“Tunategemea chakula yenye imetupwa kwenye jaa hili ata kama ni mkate au makombo ya chakula tunakula.” Familia wasema

Jaa hili laweza kuwa hifadhi ya madhara mengi kwa familia hizi, kwani wengi wao huzoa chakula, maji na kemikali nyinginezo kutoka hapa na kuzitumia wasijue athari zake. Hii ni pamoja na dawa zilizotupwa kwenye jalala kufuatia ukosefu wa hela za kupata matibabu hospitalini.

“Tukigonjeka tunatafuta dawa ndani ya chafu tunakunywa bora tu inatusaidia kesho yake tunakuwa tumepona. Wakati mwingine tunajaribu kuchanga tusaidie mwenzetu.” Familia wasema

Jalala la Charko katika eneo la Camp Garba

Uchafuzi huu wa mazingira unahatarisha si familia hizi chache tu, bali jamii nzima ya eneo la Charko, Kambi Garba. Magonjwa hatari kwa binadamu kama vile kipindupindu, homa ya matumbo, malaria na kadhalika yanaweza kuenea kutokana na jaa hili.

Kulingana na utafiti uliofanywa ni shirika moja ni kuwa watoto wachanga wako kwenye hatari zaidi ya kuambukizwa magonjwa ya mapafu kama vile pumu au asthma kutokana na kuvuta hewa chafu.

Fauka ya haya, msimu huu wa mvua husababisha jaa hili kufurika, uchafu wake ukisafirishwa na maji ya mvua hadi kwenye chemichemi nyinginezo za maji. Hii ina maana kwamba jamii inayotegemea maji ya mto pia iko hatarini.

Familia hizo zinaishutumu serikali ya kaunti kwa kuwatelekeza na wanaiomba serikali ya kaunti ya Isiolo kuwatafutia pahali mbadala pa kuishi.

“Tunaomba serikali ya kaunti watusaidie kwa kutujengea mahali pa kuishi na watoto wetu wapelekwe shuleni.” Familia wasema

Ungana nami tena siku ya Alhamisi wiki hii mwendo was aa moja, kwa sehemu ya pili ya Makala haya.

RELATED ARTICLES

WAKENYA WANA HAKI YA KUMCHAGUA KIONGOZI WANAYEMTAKA, ASKOFU IRERI ASEMA

Askofu wa jimbo katoliki la Isiolo Anthony Ireri Mukobo amewarai wananchi kufanya maamuzi mwafaka kuhusu viongozi kwa kutathmin sera na wala si...

HALI YA CORONA; IDADI YA MAAMBUKIZI

Kenya jumapili, ilirekodi visa vipya mia mbili na kimoja(201) vya maambukizi ya virusi vya corona  ikiwa ni kutoka kwa sampuli elfu nne...

NCHI YA-SAKATA UFISADI UKISALIA JINAMIZI KWA WAKENYA

Taifa la Kenya Alhamisi liliungana na ulimwengu kuadhimisha siku ya kimataifa ya vita dhidi ya ufisadi. Siku hii huadhimishwa terehe 9 mwezi...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

St. Emilie de Vialar

18th January St. Emilie de Vialar (Emily) was born in 1797 in Gaillac and ancient town in the south...

Readings at Mass Tuesday 18 January 2022

Second Week in Ordinary Time  Liturgical Colour: Green. First reading 1 Samuel 16:1-13

WENYEKITI WA BODABODA ISIOLO KUSHIRIKIANA NA VITENGO VYA USALAMA ILI KUPELEKEA KUMALIZIKA KWA UHALIFU

Muungano wa wenyekiti wa wahudumu wa bodaboda Isiolo, umesema kushirikiana Pamoja na maafisa wa  kulinda usalama, ili kumaliza uhalifu katika kaunti hii....

Msako mkali wa pombe haramu wafanyika Isiolo.

Idara ya NGAO katika kaunti ya Isiolo wamefanya msako wa pombe haramu katika eneo la Bula Pesa katika kaunti hii.