Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Local News ONYO DHIDI YA VIONGOZI WA JAMII WANAOTOA MATAMSHI YA UCHOCHEZI

ONYO DHIDI YA VIONGOZI WA JAMII WANAOTOA MATAMSHI YA UCHOCHEZI

Onyo kali limetolewa dhidi ya wanasiasa wanaotumia viongozi wa jamii kuchochea wananchi kwani watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Viongozi wa jamii mbalimbali katika kaunti ya Isiolo wamekuwa wakiidhinisha baadhi ya viongozi kuwania viti kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti, jambo ambalo huenda likachochea siasa za matabaka au misingi ya kikabila.

Akizungumza na radio shahidi kamishena wa kaunti ya Isiolo Geoffrey Omoding’ amewahimiza wanasiasa kudumisha Amani kwa kuhakikisha wanaendesha kampeni bila kuchochea wananchi.

“Naomba wanasiasa wadumishe amani wanapoendesha kampeni na wananchi wasikubali kutumika vibaya kuleta rabsha,” Omoding’ alisema,

Haya yanajiri baada ya mwenyekiti wa baraza la wazee wa jamii ya wasomali katika kaunti ya Isiolo Abdulahi Shariff kudaiwa kutoa matamshi ya uchochezi kwenye mkutano uliofanyika siku ya jumapili katika wadi ya Kinna.

Kwenye mkutano huo Shariff alichochea watu ambao ni wafuasi wa dini mojawapo kuhakikisha kwamba hawamchagui kiongozi ambaye si mfuasi wa dini hiyo, hususan kwenye kiti cha ugavana na naibu wake kwenye kaunti ya Isiolo.

Aidha Omoding’ alisema kuwa tayari uchunguzi umeanzishwa kuhusiana na kisa hicho, akiahidi kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya Shariff. Hata hivyo aliwahimiza wakaazi katika kaunti ya Isiolo kudumisha usalama.

“Nawahakikishia wananchi kuwa uchaguzi utafanyika bila tashwishi yoyote na watakaohusika na kuleta rabsha watakamatwa.”

Viongozi mbalimbali, wakiwemo wa kidini walijitokeza kukashifu matamshi yanayodaiwa kuwa ya uchochezi kutoka kwa Bw. Shariff.

Katibu wa baraza la kidini katika kaunti ya Isiolo Stephen Kalunyu aliwaomba wanasiasa kuwa mstari wa mbele kueneza amani wanapofanya kampeni zao mwaka huu.

“Tushirikiane na kitengo cha usalama kuhakikisha amani imedumishwa katika kaunti hii.”

Serikali imeahidi kuchunguza visa vyote vya matamshi ya uchochezi yanayolenga uchaguzi mkuu wa Agosti mwaka huu, huku viongozi kadha wakifunguliwa mashtaka kwa kutoa maneno ya chuki.

RELATED ARTICLES

WENYEKITI WA BODABODA ISIOLO KUSHIRIKIANA NA VITENGO VYA USALAMA ILI KUPELEKEA KUMALIZIKA KWA UHALIFU

Muungano wa wenyekiti wa wahudumu wa bodaboda Isiolo, umesema kushirikiana Pamoja na maafisa wa  kulinda usalama, ili kumaliza uhalifu katika kaunti hii....

Msako mkali wa pombe haramu wafanyika Isiolo.

Idara ya NGAO katika kaunti ya Isiolo wamefanya msako wa pombe haramu katika eneo la Bula Pesa katika kaunti hii.

Vijana 32 kaunti ya Isiolo wabadilisha mienendo yao ya matumizi ya mihadarati.

Vijana 40 katika kaunti ya Isiolo wameungana na kuunda kikundi kiitwacho "Tupendane" kwa lengo la kusaidia wasiojiweza na kuwahamasisha vijana dhidi ya...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

St. Emilie de Vialar

18th January St. Emilie de Vialar (Emily) was born in 1797 in Gaillac and ancient town in the south...

Readings at Mass Tuesday 18 January 2022

Second Week in Ordinary Time  Liturgical Colour: Green. First reading 1 Samuel 16:1-13

WENYEKITI WA BODABODA ISIOLO KUSHIRIKIANA NA VITENGO VYA USALAMA ILI KUPELEKEA KUMALIZIKA KWA UHALIFU

Muungano wa wenyekiti wa wahudumu wa bodaboda Isiolo, umesema kushirikiana Pamoja na maafisa wa  kulinda usalama, ili kumaliza uhalifu katika kaunti hii....

Msako mkali wa pombe haramu wafanyika Isiolo.

Idara ya NGAO katika kaunti ya Isiolo wamefanya msako wa pombe haramu katika eneo la Bula Pesa katika kaunti hii.