Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Local News Msako mkali wa pombe haramu wafanyika Isiolo.

Msako mkali wa pombe haramu wafanyika Isiolo.

Idara ya NGAO katika kaunti ya Isiolo wamefanya msako wa pombe haramu katika eneo la Bula Pesa katika kaunti hii.

Ni msako ambao umekuwa ukifanyika kwa muda huku idara ya usalama ikiapa kushirikiana ili kupiga marufuku pombe haramu na ulanguzi wa dawa za kulevya katika kaunti ya Isiolo.

Akizungumza na wanahabari naibu kamishna wa isiolo ya kati Joshua Otieno alisema kuwa walinasa lita 30 ya chang’aa, lita 2630 ya kangara, lita 200 ya Muna.

“Tumenasa lita 30 chang’aa, lita 2630 na lita 200 ya Muna na vifaa zaidi ya 15 vya kutengenezea na tumeshika watu wawili ambao ni Mevine Kasai na Patrick mwirigi ambao walikuwa kwa nyumba hio.” Otieno asema

Wakati uo huo Otieno aliwatahadharisha  wakaazi ambao wanaendeleza biashara ya kutengeneza pombe haramu kuwa watakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

“Serikali kuu imekataa mambo ya kutengeneza pombe haramu na ulanguzi wa dawa za kulevya na wanaoendesha biashara hizo haramu tutawakamata hivi karibuni.”

Vile vile wakaazi katika kaunti hii waliombwa kutofungua maeneo ya burudani nje yam da ulioruhusiwa huku akitoa ilani kwa wafanyibiashara walio na maeneo hayo kuhakikisha wana zingatia sheria.

“Nawatahadhari wafanyibiashara walio na maeneo ya kuuza pombe kuzingatia sheria na iwapo ungependa kufungua pahala hapo unapaswa kutembelea afisi ya idara husika kwanza.”

Tangu mwezi Januari msako wa pombe haramu ulipoanza katika kaunti hii, idara ya usalama imefanikiwa kuharibu pombe haramu lita 6,450 na vifaa Zaidi ya 30 vya kutengeneza pombe haramu.

RELATED ARTICLES

WENYEKITI WA BODABODA ISIOLO KUSHIRIKIANA NA VITENGO VYA USALAMA ILI KUPELEKEA KUMALIZIKA KWA UHALIFU

Muungano wa wenyekiti wa wahudumu wa bodaboda Isiolo, umesema kushirikiana Pamoja na maafisa wa  kulinda usalama, ili kumaliza uhalifu katika kaunti hii....

ONYO DHIDI YA VIONGOZI WA JAMII WANAOTOA MATAMSHI YA UCHOCHEZI

Onyo kali limetolewa dhidi ya wanasiasa wanaotumia viongozi wa jamii kuchochea wananchi kwani watachukuliwa hatua kali za kisheria. Viongozi...

Vijana 32 kaunti ya Isiolo wabadilisha mienendo yao ya matumizi ya mihadarati.

Vijana 40 katika kaunti ya Isiolo wameungana na kuunda kikundi kiitwacho "Tupendane" kwa lengo la kusaidia wasiojiweza na kuwahamasisha vijana dhidi ya...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

St. Emilie de Vialar

18th January St. Emilie de Vialar (Emily) was born in 1797 in Gaillac and ancient town in the south...

Readings at Mass Tuesday 18 January 2022

Second Week in Ordinary Time  Liturgical Colour: Green. First reading 1 Samuel 16:1-13

WENYEKITI WA BODABODA ISIOLO KUSHIRIKIANA NA VITENGO VYA USALAMA ILI KUPELEKEA KUMALIZIKA KWA UHALIFU

Muungano wa wenyekiti wa wahudumu wa bodaboda Isiolo, umesema kushirikiana Pamoja na maafisa wa  kulinda usalama, ili kumaliza uhalifu katika kaunti hii....

Msako mkali wa pombe haramu wafanyika Isiolo.

Idara ya NGAO katika kaunti ya Isiolo wamefanya msako wa pombe haramu katika eneo la Bula Pesa katika kaunti hii.