BARAZA LA WAZEE LAHUBIRI AMANI

0
174

Jamii zinazoendesha vita vya kijamii vinavyoendelea kulemaza shughuli za kimaisha katika kaunti za wafugaji zimetakiwa kukoma.Mwenyekiti wa baraza la Kitaifa la Wazee Phares Rutere amesema kuwa wazee wa jamii za wafugaji watakuwa wakifanya vikao vya mara kwa mara katika juhudi za kudumisha amani vilevile kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa amani.

Alikuwa akihutubia wanahabari mjini Isiolo baada ya mkutano uliousisha wazee wa jamii za kaunti za Isiolo, Meru, Marsabit na Samburu katika madhumni ya kusaidia kuleta Amani.

Matamshi yake yameungwa mkono na mwekahazina wa baraza hilo Ahmed Sett ambaye ametaka jamii iyo kuhusishwa katika masuala ya kuchunguza wanaovuruga wengine kwenye jamii.

 Sett vilevile ametaka jamii zinazofuga ngamia kutolisha maeneo ya Meru ambapo kuna wakulima