MWAKILISHI WA KINA MAMA KAUNTI YA ISIOLO AMEVUNJA KIMYA KUHUSU TOFAUTI YAKE NA VIONGOZI WENGINE

0
83

Mwakilishi wa kina mama kaunti ya Isiolo Rehema Jaldesa amevunja kimya kuhusu
tofauti zilizopo kati yake na viongozi wenzake Isiolo.
Bi Jaldesa ambaye ni mwandani wa naibu wa Rais William Ruto amesema kuwa tofauti
hizo ni za kisiasa tu.
Hapo awali, Bi Jaldesa walionekana marafiki na seneta Fatuma Dullo jambo ambalo
limebadilika kutokana na kampeni za BBI, kwani Bi Dullo anaunga mkono ripoti iyo
huku mwenzake akipinga.
Tofauti hizo zilimpelekea Bi Jaldesa kumlaki naibu wa Rais Isiolo mnamo 13 Februari,
hafla ambayo haikuhudhuria na viongozi wenzake wa Isiolo.
Hapo awali Bi Jaldesa na Bi Dullo walishirikiana kukashifu uongozi wa kaunti kwa
walichokitaja kuwa matumizi mabaya ya fedha za umma.
Hata hivyo, Bi Jaldesa anaendelea kushirikiana na Mbunge wa Isiolo Kaskazini Hassan
Odha ikidaiwa kuwa Odha anaegemea upande huo angalau anufaike kutoka kwa jamii
ya Borana kwenye uchaguzi wa 2022.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here