Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Church News Askofu Mkuu Mstaafu Lukudu Loro wa Jimbo la Juba,Sudan Kusini ameaga dunia

Askofu Mkuu Mstaafu Lukudu Loro wa Jimbo la Juba,Sudan Kusini ameaga dunia

Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu latoliki la Juba huko Sudan Kusini Paolino Lukudu Loro ameaga dunia tarehe 5 Aprili akiwa hospitali ya Nairoi Kenya.Askofu Mkuu akieleza wasifu wake marehemu amesema alikuwa nyota ya Kanisa na jamii ambayo imezimika.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Askofu Mkuu mstaafu Paolino Lukudu Loro wa Jimbo la Juba, Sudan Kusini ameaga dunia akiwa huko Nairobi Kenya mwenye umri wa miaka 80. ifa hizo zimetolewa na Mfuasi wake wa Jimbo Kuu Askofu Mkuu Stephen Ameyu,  tarehe 5 Aprili akimmwelezea kuwa Askofu Mkuu mstaafu Lukudo Loro alikuwa kama nyota ambayo imezimika.

Mchungaji huyomzee alipata kiharusi wakati alikuwa Juba, baadaye  akasafirishwa kwenda Kenya ili kutibiwa na kufia huko. “Kama mchungaji wenu ameandika Askofu Mkuu Ameyu ninwauletea habari ya kusikitisha zaidi ya maisha yangu yote. Askofu mkuu Pauline Lukudu Loro, alikuwa nyota ambaye daima ilikuwa ingaaza macho yake katika Kanisa letu na taifa letu kwa zaidi ya miaka thelathini. Habari hii ya kusikitisha haituhusu Kanisa tu, bali pia jumuiya  pana ya jamii yetu  Sudan Kusini”.

Siku nne za maombolezo zimetangazwa na kiongozi wa sasa wa Jimbo kuu la Juba. Askofu Mkuu Mstaafu Paolino Lukudo Loro alipewa daraja la kikuhani mnamo Aprili 1970. Miaka minne baadaye, aliteuliwa kuwa msimamizi wa kitume wa Jimbo la El Obeid, Sudan. Kwa maana hiyo aliteuliwa kuwa askofu wa makao hayo mnamo Mei 1979.


More Posts for Show: Radio Shahidi
RELATED ARTICLES

WAKENYA WANA HAKI YA KUMCHAGUA KIONGOZI WANAYEMTAKA, ASKOFU IRERI ASEMA

Askofu wa jimbo katoliki la Isiolo Anthony Ireri Mukobo amewarai wananchi kufanya maamuzi mwafaka kuhusu viongozi kwa kutathmin sera na wala si...

MONSIGNOR KADIMA, ATEULIWA KAMA ASKOFU MPYA WA BUNGOMA

Baba mtakatifu papa Francis Jumanne tarehe 14 December, 2021 alimteua padre Monsignor Mark Kadima kuwa askofu wa jimbo katoliki la Bungoma. Taarifa...

KANISA KATOLIKI ISIOLO LAWAFAA WATU WENYE CHANGAMOTO ZA MAUMBILE

KELVIN MWINGIRWA Mamia ya wa wakaazi wanaoishi na changamoto za ki maumbile katika eneo la kandebene iliyopo katika mpaka...

Most Popular

St. Emilie de Vialar

18th January St. Emilie de Vialar (Emily) was born in 1797 in Gaillac and ancient town in the south...

Readings at Mass Tuesday 18 January 2022

Second Week in Ordinary Time  Liturgical Colour: Green. First reading 1 Samuel 16:1-13

WENYEKITI WA BODABODA ISIOLO KUSHIRIKIANA NA VITENGO VYA USALAMA ILI KUPELEKEA KUMALIZIKA KWA UHALIFU

Muungano wa wenyekiti wa wahudumu wa bodaboda Isiolo, umesema kushirikiana Pamoja na maafisa wa  kulinda usalama, ili kumaliza uhalifu katika kaunti hii....

Msako mkali wa pombe haramu wafanyika Isiolo.

Idara ya NGAO katika kaunti ya Isiolo wamefanya msako wa pombe haramu katika eneo la Bula Pesa katika kaunti hii.

More Posts for Show: Radio Shahidi