Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Local News Mtu mmoja afariki, 40 wengine hospitalini baada ya kula mzoga wa ngamia...

Mtu mmoja afariki, 40 wengine hospitalini baada ya kula mzoga wa ngamia Isiolo.

Na Jackline Mung’athia

Mtu mmoja amefariki huku wengine 40 wakiendelea kupokea matibabu katika hospitali za mbali mbali ikiwemo hospitali ya rufaa ya Isiolo baada yao kula mzoga wa ngamia wikendi katika eneo la Oldonyiro kaunti ya Isiolo.

Akidhibitisha kisa hicho kamishna wa kaunti ya Isiolo Herman Shambi amewashauri wakaazi kutokula nyama ya mnyama aliyekufa na badala yake kutafuta usaidizi kutoka kwa afisaa wa afya wa mifugo au kumzika mnyama huyo. Vile vile Shambi amewashukuru maafisa wa afya kwa kazi nzuri waliyofanya kuwahudumia wakaazi hao na kuhakikisha kuwa wameokoa maisha yao.

Aidha mwakilishi wa wadi hiyo David Lemantile amesema kuwa wagonjwa 14 wamepelekwa katika hospitali ya rufaa ya Isiolo na wanaendelea kuhisi vyema. Lemantile amewaomba waliosalia nyumbani kusaka matibabu hospitalini badala ya kutumia dawa ya miti shamba au wafariki.

(Kwa maoni, swali au malalamishi wasiliana nasi kupitia 0746113746)

RELATED ARTICLES

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Mwanaume apatikana ameuwawa eneo la Redcross

Hali ya woga imetanda katika eneo la Redcross wadi ya Bullapesa,kaunti ya Isiolo, hii ni baada ya mwili wa mwanamume mmoja mwenye...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Readings at Mass Tuesday 7 September 2021

23rd Sunday in Ordinary Time  Liturgical Colour: Green. First reading Colossians 2:6-15

Blessed Frederic Antoine Ozanam

7TH SEPT Antoine-Frederic Ozanam was an ordinary guy with extraordinary talent who lived an ordinary life but loved in...