Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Local News GAVANA WA WAJIR AAHIDI KUIMARISHA SEKTA YA AFYA, MAJI NA ELIMU

GAVANA WA WAJIR AAHIDI KUIMARISHA SEKTA YA AFYA, MAJI NA ELIMU

Gavana mpya wa Wajir Ahmed Ali Muktar amesema kwamba atazipa kipaumbele sekta za Maji, afya na Elimu katika utawala wake. Kando na hayo, Muktar aliongeza kwamba serikali yake pia itaangazia suala la usalama na ukosefu wa amani, pamoja na Kuunganisha wananchi wa Garissa

Muktar aliapishwa wiki iliyopita, punde tu baada ya kung’atuliwa kwa aliyekuwa gavana wa kaunti hiyo Mohamed Abdi Mohamud. Wawakilishi wadi wa bunge la Wajir walipiga kura ya kumwengua Mohamud kwa shutuma za matumizi mabaya ya afisi na utendakazi mbaya.

Kwenye mahojiano na runinga ya humu nchini siku ya jumanne, Muktar alisema kwamba mtangulizi wake aliacha msururu wa madeni, hivyo atalazimika kuyalipa kwanza wakati wakazi wa Wajir wakiendelea kusubiri kukamilishwa kwa miradi.

Hata hivyo gavana huyo, alidokeza kwamba kwa sasa hospitali nyingi na zahanati zilizoko kwenye kaunti ya Wajir zimerejelea shughuli zake baada ya wahudumu wa afya kukutana na gavana huyo mpya, na kuwasilisha malalamishi yao.

Mukhtar alisema kwamba waliafikiana kuhusu jinsi ya kutatua baadhi ya matatizo ya madaktari na wauguzi.

Gavana Muktar alirithi afisi hiyo licha ya ombi lililowasilishwa mahakamani na gavana Mohamud kuzuia uapisho wake. Siku ya jumanne tarehe 25 Mei, mahakama ya Meru ilipeana kesi hiyo kwa jaji mkuu Martha Koome ikimwomba ateue jopo la majaji watatu kuamua kesi hiyo.

RELATED ARTICLES

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Mwanaume apatikana ameuwawa eneo la Redcross

Hali ya woga imetanda katika eneo la Redcross wadi ya Bullapesa,kaunti ya Isiolo, hii ni baada ya mwili wa mwanamume mmoja mwenye...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Readings at Mass Tuesday 7 September 2021

23rd Sunday in Ordinary Time  Liturgical Colour: Green. First reading Colossians 2:6-15

Blessed Frederic Antoine Ozanam

7TH SEPT Antoine-Frederic Ozanam was an ordinary guy with extraordinary talent who lived an ordinary life but loved in...