Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Church News KANISA LAKASHIFU VIONGOZI KUHUSU CHECHE ZA MANENO DHIDI YA MAHAKAMA

KANISA LAKASHIFU VIONGOZI KUHUSU CHECHE ZA MANENO DHIDI YA MAHAKAMA

Kanisa Alhamisi 27 Mei lilipeana wosia wake kuhusu mdahalo unaoendelea nchini baada ya uamuzi wa mahakama kuharamisha mchakato wa kuifanyia marekebisho katiba kupitia kura ya maoni.

Kwenye taarifa, baraza la maaskofu wa kanisa katoliki KCCB lilitoa mwito kwa viongozi kukoma kukashifu mahakama.

Kanisa lilisema kwamba hisia zinazoendelea kuibuliwa na baadhi ya viongozi ni kuhujumu uhuru wa idara ya mahakama.

Kupitia barua iliyotiwa saini na mwenyekiti wa KCCB Askofu Martin Kivuva Musonde kwa niaba ya maaskofu wote, kanisa lilionya kwamba kuna uwezekano mkubwa kwamba kura ya maoni haitawezekana kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2022. Kwa sababu hii, kanisa liliomba kwamba pasiwepo na mpango wowote wa kuahirisha uchaguzi mkuu wa mwaka 2022, kwa ajili ya kura ya maoni.

Wakati uo huo, kanisa limesikitishwa na mvutano uliopo kati ya serikali kuu na idara ya mahakama. KCCB iliomba zoezi la kuapisha majaji 41 kuharakishwa ili kusuluhisha dhiki ya mrundiko wa kesi mahakamani.

Maaskofu wa kanisa katoliki wamesema haya kwenye taarifa ya pamoja kuhusu hali ya taifa. Miongoni mwa mapendekezo mengine waliyotoa ni pamoja na kuimarisha tume ya uchaguzi IEBC kupitia mabadiliko yafaayo na kwa kuteuwa makamisena wengine kujaza nafasi zilizoachwa wazi ndani ya tume hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ni jambo la kusikitisha na aibu kwamba hadi leo nafasi za makamishena hao hazijaweza kujazwa. Taarifa hiyo ya maaskofu wa kanisa katoliki limejiri wakati ambapo kumekuwapo na hisia kali miongoni mwa wanasiasa na viongozi wakuu serikalini kuhusu uamuzi wa mahakama kuu kuitaja BBI kama ukiukaji wa katiba.

Hata hivyo baadhi ya viongozi akiwemo rais Uhuru Kenyatta na Kiongozi wa ODM Raila Odinga waliwasilisha rufaa mahakamani wakitaka uamuzi huo ubadilishwe. Taarifa ya Maaskofu iliongozwa na kauli mbilu “Kwa ujasiri na matumaini sote tutasimama.”

RELATED ARTICLES

SHANGWE ZARINDIMA SHEREHE ZA MTAKATIFU EUSEBIUS ISIOLO

Na Tracy Nakato Parokia ya  mt. eusebius, jumapili imesherehekea siku kuu ya familia ambayo imemsherehekea mtakatifu Eusebius. Mtakatifu Eusebius...

ASKOFU MUKOBO AONYA DHIDI YA KUHAIRISHA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2022

Kanisa limeendelea kuhimiza umuhimu wa kura ya maoni kufanyika baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 na si kabla. Akiongea wakati wa...

REMEMBERING LUIGI LOCATI, FIRST BISHOP OF ISIOLO

At the geographical heart of Kenya, below the scorching sun of the northern   part of Kenya, stands the twin rectangular towers, that...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Readings at Mass Tuesday 7 September 2021

23rd Sunday in Ordinary Time  Liturgical Colour: Green. First reading Colossians 2:6-15

Blessed Frederic Antoine Ozanam

7TH SEPT Antoine-Frederic Ozanam was an ordinary guy with extraordinary talent who lived an ordinary life but loved in...