Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Church News KWA NINI KUFUNGA MAKANISA? MAASKOFU WA KANISA KATOLIKI WALALAMIKA

KWA NINI KUFUNGA MAKANISA? MAASKOFU WA KANISA KATOLIKI WALALAMIKA

Kanisa limesikitishwa na hatua ya serikali la kufunga maeneo ya ibada kila wakati kunapokuwa na mkurupuko wa virusi hivyo katika baadhi ya maeneo, ilhali maeneo mengineo ya uma yanaruhusiwa kuendesha shughuli zake.

Kupitia barua iliyotiwa saini na mwenyekiti wa baraza la maaskofu wa kanisa katoliki nchini kenya KCCB Askofu Martin Kivuva Musonde, maaskofu wamelalamika kwamba viongozi wa kisiasa pia wangali wanaendesha mikutano ya kisiasa na huenda ikachangia katika kuenea kwa Covid-19.

“inauma sana kuona kwamba maeneo ya ibada yanafungwa kila wakati, huku kwingineko watu wanaendesha shughuli zao bila kuzingatia maagizo yoyote ya wizara ya afya kuhusu kuzuia msambao wa Corona”

Kanisa halijasita kuwakosoa maafisa wa usalama wanaowaangaisha wananchi wakati wa kutekeleza sheria za kuzuia msambao wa virusi nchini. Kwa mujibu wa KCCB, hii ni kukiuka haki za binadamu.

“kuna njia mbadala za kutekeleza maagizo ya serikali bila kuhujumu haki za binadamu. Visa vimeripotiwa vya maafisa wa polisi kuingia kwenye maeneo ya ibada na kuwanyanyasa waumini. Maeneo ya ibada yanafaa kuheshimiwa na kila mtu.”

Kando na hayo kanisa limetoa mwito kwa serikali na mashirika ya wahisani kutuma chakula cha msaada kwa wakenya ambao wameathiriwa na mafuriko ya mvua nchini, ambapo takriban watu elfu 25 wamelazimika kuhama makwao huku wengi wakiaga dunia.

Kwa sasa takriban wakenya milioni kwenye maeneo kame nchini 1.4 wanakumbwa na janga la njaa, huku kanisa sasa likiitaka serikali kubuni mikakati ya kudumu ili kuzuia majanga yanayotokana na hali hii.

RELATED ARTICLES

SHANGWE ZARINDIMA SHEREHE ZA MTAKATIFU EUSEBIUS ISIOLO

Na Tracy Nakato Parokia ya  mt. eusebius, jumapili imesherehekea siku kuu ya familia ambayo imemsherehekea mtakatifu Eusebius. Mtakatifu Eusebius...

ASKOFU MUKOBO AONYA DHIDI YA KUHAIRISHA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2022

Kanisa limeendelea kuhimiza umuhimu wa kura ya maoni kufanyika baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 na si kabla. Akiongea wakati wa...

REMEMBERING LUIGI LOCATI, FIRST BISHOP OF ISIOLO

At the geographical heart of Kenya, below the scorching sun of the northern   part of Kenya, stands the twin rectangular towers, that...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Readings at Mass Tuesday 7 September 2021

23rd Sunday in Ordinary Time  Liturgical Colour: Green. First reading Colossians 2:6-15

Blessed Frederic Antoine Ozanam

7TH SEPT Antoine-Frederic Ozanam was an ordinary guy with extraordinary talent who lived an ordinary life but loved in...