Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Local News WATU WAWILI WAFARIKI HOSPITALINI HUKU WAUGUZI WAKISHEREHEKEA 'BIRTHDAY'

WATU WAWILI WAFARIKI HOSPITALINI HUKU WAUGUZI WAKISHEREHEKEA ‘BIRTHDAY’

Familia mbili mjini Nanyuki, kaunti ya Laikipia wanalilia haki baada ya wagonjwa wawili kudaiwa kufariki walipokuwa kwa kukosa matibabu katika hospitali ya rufaa ya Nanyuki.

Wanasema kwamba wahasiriwa walipoteza maisha yao kwa kukosa kuhudumiwa, licha ya kuwa wahudumu wa hospitali hiyo walikuwa wakisherehekea siku ya kuzaliwa – yaani Birthday.

Familia ya mwendazake Halima Hassan mwenye umri wa miaka 58, imelalama kwamba mwasiriwa alikuwa amepelekwa hospitalini humo akiwa na matatizo ya shinikizo la damu. Hata hivyo alikosa wa kumhudumia kwani wauguzi walikuwa wakiandaa sherehe za mmoja wao kwenye mahabara ya hospitali.

Wakati uohuo, mwasiriwa mwingine, Jane Njoki Ichuga amedaiwa kufariki dunia baada ya kuvuja damu nyingi baada ya kujifungua hospitalini humo.

Ibrahim Mohammed, mumewe Njoki, anasema kwamba familia ilikuwa imejiandaa kuchangia damu kuokoa maisha yake, ikiwalazimu kununua hata dawa nje ya hospitali hiyo kwani wauguzi waliwaambia kwamba hawafanyi kazi wakati wa sikukuu.

Hata hivyo Mohammed anasema kwamba aligundua baadaye kwamba wauguzi hao walikuwa wakisherehekea siku ya kuzaliwa kwa mmoja wao.

Gavana wa Laikipia Ndiritu Muriithi amekiambia kituo kimoja cha habari hapa nchini kwamba uchunguzi umeanzishwa kufuatia madai hayo.

RELATED ARTICLES

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Mwanaume apatikana ameuwawa eneo la Redcross

Hali ya woga imetanda katika eneo la Redcross wadi ya Bullapesa,kaunti ya Isiolo, hii ni baada ya mwili wa mwanamume mmoja mwenye...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Readings at Mass Tuesday 7 September 2021

23rd Sunday in Ordinary Time  Liturgical Colour: Green. First reading Colossians 2:6-15

Blessed Frederic Antoine Ozanam

7TH SEPT Antoine-Frederic Ozanam was an ordinary guy with extraordinary talent who lived an ordinary life but loved in...