Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Church News KANISA KATOLIKI LASISITIZA HAJA YA VIONGOZI KUHESHIMU SHERIA

KANISA KATOLIKI LASISITIZA HAJA YA VIONGOZI KUHESHIMU SHERIA

Kanisa limeendelea kusisitiza haja ya viongozi na asasi za serikali kuheshimu sheria. Ni maafikio yaliyotangazwa na maaskofu wa kanisa katoliki nchini Kenya mnamo tarehe 27 mei mwaka huu.

Akirejelea taarifa hiyo ya baraza la maaskofu KCCB, Askofu ya jimbo katoliki la Isiolo Antony Ireri Mukobo amesema idara zote za serikali ikiwemo mahakama, bunge na afisi kuu zinafaa kuheshimiana na kutii sheria.

Kauli ya askofu inajiri huku kukiwa na baadhi ya viongozi wanaoirushia cheche za maneno idara ya mahakama kufuatia uamuzi wa kukataa marekebisho ya katiba kuitia kura ya maoni BBI. Askofu Ireri amesema kwamba idara zote tatu za serikali zinapaswa kufanya kazi kwa pamoja na kwa uuwiano bila kuhujumiana.

Kadhalika, askofu Ireri ameshikilia msimamo wa kanisa katoliki kwamba marekebisho ya katiba yanayopendekezwa yanafaa kufanywa baada ya uchaguzi na wala si kabla yake, ili yasije yakavuruga Amani nchini.

Ameyasema haya wakati wa ibada ya misa ya jumapili. Ikumbukwe kwamba tarehe 27 mwezi uliopita kupitia taarifa ya pamoja, baraza maaskofu wa kanisa katoliki lilitoa mwelekeo kuhusu masuala kadha, yakiwemo ya uongozi, uchaguzi mkuu na kura ya maoni, janga la Korona, hali ya njaa nchini na uuwiano wa kitaifa.

RELATED ARTICLES

SHANGWE ZARINDIMA SHEREHE ZA MTAKATIFU EUSEBIUS ISIOLO

Na Tracy Nakato Parokia ya  mt. eusebius, jumapili imesherehekea siku kuu ya familia ambayo imemsherehekea mtakatifu Eusebius. Mtakatifu Eusebius...

ASKOFU MUKOBO AONYA DHIDI YA KUHAIRISHA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2022

Kanisa limeendelea kuhimiza umuhimu wa kura ya maoni kufanyika baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 na si kabla. Akiongea wakati wa...

REMEMBERING LUIGI LOCATI, FIRST BISHOP OF ISIOLO

At the geographical heart of Kenya, below the scorching sun of the northern   part of Kenya, stands the twin rectangular towers, that...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Readings at Mass Tuesday 7 September 2021

23rd Sunday in Ordinary Time  Liturgical Colour: Green. First reading Colossians 2:6-15

Blessed Frederic Antoine Ozanam

7TH SEPT Antoine-Frederic Ozanam was an ordinary guy with extraordinary talent who lived an ordinary life but loved in...