Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Local News "Gavana kuti, Kamilisha ahadi yako," wasema viongozi wa vijana

“Gavana kuti, Kamilisha ahadi yako,” wasema viongozi wa vijana

Na Mureithi Kirimi

Viongozi wa mradi wa kazi mtaani, wameitaka serikali ya kaunti kuanzisha miradi ambayo itawasaidia vijana wakati mradi wa kazi mtaani utakapokamilika. aidha wamewakashifu viongozi pamoja na serikali ya kaunti ya Isiolo wakisema kuwa hawajakuwa wakiyashughulikia maswala ya vijana ata baada ya gavana Mohamed Abdi Kuti kuwaahidi usaidizi.

Kadhalika, viongozi hao wameiomba serikali kuu kuongeza mda wa mradi wa kazi mtaani, ili uweze kuwafaidi vijana zaidi.

Wakiongea na wanahabari mjini Isiolo mwenyekiti wa mradi wa kazi mtaani Adan hassan akiandamana na viongozi wenzake, wamesema kuwa mradi huo umewasaidia vijana pakubwa na hivyo kuna haja ya kuongezewa muda kwani unanuiwa kukamilika siku ya alamisi wiki hii.

Mradi huo ambao uliwasaidia vijana Zaidi ya 3000 katika kaunti ya Isiolo, ulianzishwa naye Rais Uhuru Kenyatta ili kuwasaidia vijana ambao walipoteza kazi kutokana na janga la korona na pia kuwasaidia vijana kuepukana na uhalifu kama vile utumizi wa dawa za kulevya.
 
RELATED ARTICLES

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Mwanaume apatikana ameuwawa eneo la Redcross

Hali ya woga imetanda katika eneo la Redcross wadi ya Bullapesa,kaunti ya Isiolo, hii ni baada ya mwili wa mwanamume mmoja mwenye...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Readings at Mass Tuesday 7 September 2021

23rd Sunday in Ordinary Time  Liturgical Colour: Green. First reading Colossians 2:6-15

Blessed Frederic Antoine Ozanam

7TH SEPT Antoine-Frederic Ozanam was an ordinary guy with extraordinary talent who lived an ordinary life but loved in...