Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News National News SERIKALI YAPONGEZA KANISA KATOLIKI KWA JUHUDI ZA KUBORESHA MAZINGIRA

SERIKALI YAPONGEZA KANISA KATOLIKI KWA JUHUDI ZA KUBORESHA MAZINGIRA

Wizara ya mazingira na misitu nchini imepongeza azma ya kanisa katoliki la kupanda miti ili kuafikia asilimia 10 ya ardhi iliyo na miti nchini.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa mpango wa Environment Kenya, Katibu wa kudumu kwenye wizara hiyo Dr Chris Kiptoo amesema kuwa mchango wa kanisa katoliki katika maendeleo ya nchi ni mkubwa, haswa ikizingatiwa kwamba kanisa hili lina mashule na makanisa kote nchini na mamilioni ya waumini ambao watasaidia katika kuhakikisha azimio la mazingira bora.

Kwa mujibu wa wizara ya mazingira na misitu, kanisa katoliki litahamasisha mashule, parokia na taasisi zake kuzalisha miche milioni 50 ili kusadia upanzi wa miti kwenye mazingira yao chini ya mpango wa Enviroment Kenya.

Wizara hiyo imetia saini mkataba wa kushirikiana na kanisa katoliki katika kuafikia asilimia 10 ya ardhi iliyo na miti nchini Kenya.

RELATED ARTICLES

RAIS KENYATTA AANDAA MKUTANO BAINA YA RAILA NA VINARA WA ONE KENYA

Rais Uhuru Kenyatta leo amekutana na viongozi watano wa vyama vya kisiasa humu nchini. Ni mkutano ambao umekisiwa wa kujaribu kuwaunganisha Raila...

KAUNTI ZOTE ZIWE NA MAHAKAMA KUU, ASEMA JAJI MKUU

Jaji mkuu Martha Koome amesisitiza haja ya kaunti zote nchini kuwa na mahakama kuu. Koome ameiambia baraza la magavana kwamba majimbo saba...

MWANAUME ANAYEDAIWA KUWATEKA NYARA NA KUUWA WATOTO 10 AKAMATWA NAIROBI

Makachero wa uchunguzi wa jinai DCI wanamzuilia mwanaumwe mwenye umri wa miaka 20 anayeshukiwa kuwateka nyara na kuwaua watoto mjini Nairobi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Readings at Mass Tuesday 7 September 2021

23rd Sunday in Ordinary Time  Liturgical Colour: Green. First reading Colossians 2:6-15

Blessed Frederic Antoine Ozanam

7TH SEPT Antoine-Frederic Ozanam was an ordinary guy with extraordinary talent who lived an ordinary life but loved in...