Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News National News SERIKALI YAONGEZA AMRI YA KAFYU KWA BAADHI ZA KAUNTI NCHINI

SERIKALI YAONGEZA AMRI YA KAFYU KWA BAADHI ZA KAUNTI NCHINI

Serikali imeongeza muda wa marufuku ya kutotoka nje wakati wa usiku almaarufu kafyu kwenye kaunti 13 humu nchini.

Kuanzia kesho ijumaa tarehe 18th Juni, wakazi wa mkoa wa Nyanza, Bonde la Ufa na Magharibi watalazimika kusalia nyumbani kwao kuanzia saa moja jioni hadi saa kumi asubuhi.

Wizara ya afya imesema kwamba hatua hii ni katika jitihada za kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya Corona kwenye maeneo hayo. Kaunti zitakazoadhirika ni Kisumu, Siaya, Homabay, Migori, Trans-Nzoia, Bomet, Kericho, Bungoma, Nyamira, Kisii, Vihiga, Kakamega na Busia.

Kwa mujibu wa waziri wa afya Mutahi Kagwe, maeneo hayo yameandikisha ongezeko la maambukizi ya ugonjwa wa Covid 19 kwa asilimia 21, huku maeneo mengine ya nchi yakiandikisha asilimia tisa. Kadhalika, serikali pia imepiga marufuku shughuli zote za ibada kwenye kaunti hizo 13.

RELATED ARTICLES

RAIS KENYATTA AANDAA MKUTANO BAINA YA RAILA NA VINARA WA ONE KENYA

Rais Uhuru Kenyatta leo amekutana na viongozi watano wa vyama vya kisiasa humu nchini. Ni mkutano ambao umekisiwa wa kujaribu kuwaunganisha Raila...

KAUNTI ZOTE ZIWE NA MAHAKAMA KUU, ASEMA JAJI MKUU

Jaji mkuu Martha Koome amesisitiza haja ya kaunti zote nchini kuwa na mahakama kuu. Koome ameiambia baraza la magavana kwamba majimbo saba...

MWANAUME ANAYEDAIWA KUWATEKA NYARA NA KUUWA WATOTO 10 AKAMATWA NAIROBI

Makachero wa uchunguzi wa jinai DCI wanamzuilia mwanaumwe mwenye umri wa miaka 20 anayeshukiwa kuwateka nyara na kuwaua watoto mjini Nairobi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Readings at Mass Tuesday 7 September 2021

23rd Sunday in Ordinary Time  Liturgical Colour: Green. First reading Colossians 2:6-15

Blessed Frederic Antoine Ozanam

7TH SEPT Antoine-Frederic Ozanam was an ordinary guy with extraordinary talent who lived an ordinary life but loved in...