Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Local News WAFANYIBIASHARA MJINI ISIOLO WALALAMIKA BAADA YA KUFUNGIWA SOKO

WAFANYIBIASHARA MJINI ISIOLO WALALAMIKA BAADA YA KUFUNGIWA SOKO

Wafanyibiashara katika kaunti ya Isiolo wameonesha kukerwa na tukio la kunyimwa idhini ya kuendeleza biashara katika soko kuu mjini Isiolo. Wafanyibiashara hao haswa wanaopakia mizigo almaarufu Beba beba wamelalamikia ukosefu wa ajira tangu soko hiyo ilipofungwa.

Akizungumza na Radio shahidi, mwenyekiti wa chama cha vijana wa Beba beba katika soko ya Isiolo Kassim Juma amesema kuwa ukosefu wa ajira na mapato kufuatia kufungwa soko ya Jumatatu, Alhamisi na Ijumaa utawapelekea vijana kujihusisha na uhalifu.

Wakati uo huo, vijana hao wameeleza hofu yao kwamba kutokana na ukosefu wa ajira, idadi ya watoto wanaorandaranda mitaani huenda ikaongezeka. Vijana hao wameomba serikali ya kaunti kutafuta suluhu ya kudumu ili wapate ajira kama njia moja ya kupunguza uhalifu.

Hata hivyo, Meneja wa manispaa ya Isiolo Osman Halake amewaomba wafanyabiashara waliopoteza ajira kuwa wavumilivu kwani kufikia tarehe mosi mwezi julai watakuwa wameweka mikakati dhabiti na kupata suluhu la kudumu.

RELATED ARTICLES

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Mwanaume apatikana ameuwawa eneo la Redcross

Hali ya woga imetanda katika eneo la Redcross wadi ya Bullapesa,kaunti ya Isiolo, hii ni baada ya mwili wa mwanamume mmoja mwenye...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

Mashabiki wa radio Shahidi, wawatunuku wanafunzi wa Shule ya kambi ya Juu kwa madawati

Radio shahidi kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi na mashabiki wametoa ufadhili wa madawati thelathini na matatu,  katika shule ya msingi ya...

Wakaazi wa Burat Isiolo wawasilsha malalamishi kwa NLC.

Wakaazi wa wadi ya Burat kaunti ya Isiolo wamewasilisha malalamishi yao katika afisi ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi kufuatia dhuluma za...

Readings at Mass Tuesday 7 September 2021

23rd Sunday in Ordinary Time  Liturgical Colour: Green. First reading Colossians 2:6-15

Blessed Frederic Antoine Ozanam

7TH SEPT Antoine-Frederic Ozanam was an ordinary guy with extraordinary talent who lived an ordinary life but loved in...