Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home Uncategorized Bunge La Kaunti Ya Marsabit Limekuwa La Hivi Punde Kupitisha Mswaada Wa...

Bunge La Kaunti Ya Marsabit Limekuwa La Hivi Punde Kupitisha Mswaada Wa Marekebisho Wa Mwaka Wa 2020.

Bunge la Kaunti ya  Marsabit limekuwa la hivi punde kupitisha mswaada wa marekebisho wa mwaka wa 2020.

Mswada huo wa marekebisho ya katiba kupitia mpango wa maridhiano ya kitaifa BBI umewasilishwa katika bunge hilo hii leo na kupitishwa na MaMCAs 24 bila kupingwa na yeyote.

Aidha ni MaMCAs 6 pekee waliokosa kuhudhuria kikao cha leo.

Awali, Bunge la Kaunti ya Marsabit lilikuwa limetoa nafasi kwa umma kutoa maoni yao kuhusu mswada huo kufikia hiyo jana.

Waliouga Mkono mswaada huo wametaja kuwa maswala ya mizozo ya mara kwa mara ambayo hushuhudiwa kila baada ya uchaguzi yatakuwa yakale.

VileVile wamesifia ongezeko la fedha kuelekea kwa majimbo huku wakitaja kuwa mandeleo zaidi yatashuhudiwa mashinani.

Tayari mswada huo umetimiza uungwaji mkono wa mabunge 24 yanayohitajika kikatiba ili uelekezwe katika Bunge la Kitaifa kujadiliwa.

Kufikia sasa Mabunge ya kaunti 32 yamepitisha mswaada huo Bunge la kaunti ya Baringo likiwa ndilo la kipekee kuupinga.

RELATED ARTICLES

St. Germanus of Paris

Germain was born near Autun in what is now France, under Burgundian control 20 years after the collapse of the Western Roman...

READINGS AT MASS FRIDAY 28 MAY 2021

 Readings at Mass Friday 28 May 2021 Eighth Week in Ordinary Time Liturgical...

RADIO SHAHIDI YANG’AA KATIKA KUZA AWARDS 2021

Kituo cha Radio Shahidi kwa mara nyingine kimeibuka kituo bora katika upeperushaji wa matangazo bora ya elimu kwa jamii haswa wakati huu...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

Makadirio ya uzalishaji wa chakula katika sekta ya Ukulima

Mazao ya vyakula yanatarajiwa kuongezeka kati ya mwaka wa 2018 hadi 2022 Ongezeko hili linatarajiwa   kufuatia vijana katika kaunti...

Sen. Abshiro aitaka serikali ya Isiolo kuzisaidia hifadhi za jamii.

Seneta mteule Halake Abshiro, ameitaka serikali ya kaunti ya Isiolo kutenga fedha Zaidi  katika bajeti yake kwa manufaa ya wakaazi wanaoishi katika...

NYOTA YA MATUMAINI KWA VIJANA WANAOITAJI KUJIKIMU NA KOZI ZA KIUFUNDI

Huku Kenya ikizidi kufanikisha ruwaza ya mwaka wa elfu mbili na thelathini, vijana wanazidi kutakiwa kujikimu na ujuzi wa kiteknikali ili waweze...

Makadirio ya mapato ya Kaunti ya Isiolo.

Mapato ya Kaunti ya Isiolo yanatarajiwa kuongezeka kati ya 2017-2022.  Ongezeko hili linatarajiwa kuwa thabiti. Mwaka wa 2017/18...