Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Mwanaume ashtakiwa kwa kusafirisha bangi Isiolo.

Mwanaume ashtakiwa kwa kusafirisha bangi Isiolo.

By Jackline Mung’athia, 21st April 2021

Mwanaume wa umri wa makamo amefikishwa kwenye mahakama ya Isiolo Jumatano na kushtakiwa kwa kosa la kupatikana akisafirisha bangi.

Mohammed Adano amefikishwa mbele ya hakimu mkuu Samuel Mungai kwa shtaka la kusafirisha bangi kilo 18.25.

Kulingana na ushahidi uliotolewa na polisi kutoka kitengo cha upelelezi CID, ni kuwa mnamo tarehe 26 Februari mwaka huu, Adano alipatikana na bangi iliyokuwa ndani ya trela, katika kizuizi cha Archers post.

Aidha mmiliki wa gari ambalo Adano alikuwa akiendesha amesema kuwa gari lake hutumika kusafirisha chupa kutoka Ethiopia hadi Nairobi na hakuwa na ufahamu wa iwapo Adano amekuwa akisafirisha bangi.

Hakimu mkuu Samuel Mungai ameamuru mshtakiwa na mashahidi kuandamana hadi katika kituo cha polisi cha Isiolo ambapo trela hiyo imezuiliwa, ili kudhibitisha kama ndilo lililonaswa likisafirisha bangi hiyo.

RELATED ARTICLES

St. Germanus of Paris

Germain was born near Autun in what is now France, under Burgundian control 20 years after the collapse of the Western Roman...

READINGS AT MASS FRIDAY 28 MAY 2021

 Readings at Mass Friday 28 May 2021 Eighth Week in Ordinary Time Liturgical...

RADIO SHAHIDI YANG’AA KATIKA KUZA AWARDS 2021

Kituo cha Radio Shahidi kwa mara nyingine kimeibuka kituo bora katika upeperushaji wa matangazo bora ya elimu kwa jamii haswa wakati huu...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

Makadirio ya uzalishaji wa chakula katika sekta ya Ukulima

Mazao ya vyakula yanatarajiwa kuongezeka kati ya mwaka wa 2018 hadi 2022 Ongezeko hili linatarajiwa   kufuatia vijana katika kaunti...

Sen. Abshiro aitaka serikali ya Isiolo kuzisaidia hifadhi za jamii.

Seneta mteule Halake Abshiro, ameitaka serikali ya kaunti ya Isiolo kutenga fedha Zaidi  katika bajeti yake kwa manufaa ya wakaazi wanaoishi katika...

NYOTA YA MATUMAINI KWA VIJANA WANAOITAJI KUJIKIMU NA KOZI ZA KIUFUNDI

Huku Kenya ikizidi kufanikisha ruwaza ya mwaka wa elfu mbili na thelathini, vijana wanazidi kutakiwa kujikimu na ujuzi wa kiteknikali ili waweze...

Makadirio ya mapato ya Kaunti ya Isiolo.

Mapato ya Kaunti ya Isiolo yanatarajiwa kuongezeka kati ya 2017-2022.  Ongezeko hili linatarajiwa kuwa thabiti. Mwaka wa 2017/18...