Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News MWAKILISHI WA BABA MTAKATIFU AZURU JIMBO LA ISIOLO

MWAKILISHI WA BABA MTAKATIFU AZURU JIMBO LA ISIOLO

By: Henry Mwangangi and Felix Mulei

Mwakilishi wa baba mtakatifu nchini Kenya Askofu mkuu Hurbatus Van Megen Ijumaa alizuru Jimbo katoliki la Isiolo na kupokelewa na askofu Anthony Ireri Mukobo.

Punde tu baada ya kuwasili, Van Megen alitembelea hospitali ya Matter care, parokia ya Our Lady of Assumption Kambi ya Juu na vile vile makao makuu ya dayosisi ya kanisa katoliki mjini Isiolo kwenye kathedrali ya Mtakatifu Eusebio akiwa ameandamana na askofu Mukobo na mapadre wengine.

Akizungumza na waumini katika parokia ya Kambi ya Juu Nuncio Van Megen amewashukuru kwa kujitolea kwa kazi ya Mungu na kuelezea furaha yake kuwa Isiolo.

Kwa upande wao, waumini wamejawa na furaha kutembelewa na mwakilishi huyo wa baba mtakatifu Francis wakiitaja ziara ya Nuncio kama yenye Baraka kuu.

Baadaye alasiri, Nuncio Van Megen alitoa heshima zake kwenye kaburi la askofu mwanzilishi wa jimbo la Isiolo, Luigi Locatti.

Nuncio Van Megen yumo kwenye ziara rasmi ya kitume kwenye jimbo katoliki la Isiolo ambapo atatembelea pia baadhi ya parokia na taasisi nyinginezo.

Jumapili ijayo, atazuru Radio Shahidi na kuzungumza kwenye kipindi cha asubuhi, kabla ya kusherehekea misa ya jumapili.

Kilele cha ziara yake kitakuwa ni kusherehekea misa ya kuadhimisha miaka 40 ya upadre na miaka 20 ya uaskofu wa askofu Ireri, ambapo pia atazindua rasmi jarida la jimbo kwa jina Shahidi Newsletter, mitandao ya kijamii na wavuti rasmi wa jimbo.

RELATED ARTICLES

Mwanaume ashtakiwa kwa kusafirisha bangi Isiolo.

By Jackline Mung’athia, 21st April 2021 Mwanaume wa umri wa makamo amefikishwa kwenye mahakama ya Isiolo Jumatano na kushtakiwa...

WAKAAZI WAPUUZA MIKAKATI YA WIZARA YA AFYA

Zaidi ya watu kumi wamepoteza maisha yao kutokana na maambukizi ya virusi vya corona katika kaunti ya Isiolo tangu kuripotiwa kwa...

Most Popular

Makadirio ya uzalishaji wa chakula katika sekta ya Ukulima

Mazao ya vyakula yanatarajiwa kuongezeka kati ya mwaka wa 2018 hadi 2022 Ongezeko hili linatarajiwa   kufuatia vijana katika kaunti...

Sen. Abshiro aitaka serikali ya Isiolo kuzisaidia hifadhi za jamii.

Seneta mteule Halake Abshiro, ameitaka serikali ya kaunti ya Isiolo kutenga fedha Zaidi  katika bajeti yake kwa manufaa ya wakaazi wanaoishi katika...

NYOTA YA MATUMAINI KWA VIJANA WANAOITAJI KUJIKIMU NA KOZI ZA KIUFUNDI

Huku Kenya ikizidi kufanikisha ruwaza ya mwaka wa elfu mbili na thelathini, vijana wanazidi kutakiwa kujikimu na ujuzi wa kiteknikali ili waweze...

Makadirio ya mapato ya Kaunti ya Isiolo.

Mapato ya Kaunti ya Isiolo yanatarajiwa kuongezeka kati ya 2017-2022.  Ongezeko hili linatarajiwa kuwa thabiti. Mwaka wa 2017/18...