Ooops ! You forgot to enter a stream url ! Please check Radio Player configuration

Home News Church News KANISA KATOLIKI LASISITIZA HAJA YA VIONGOZI KUHESHIMU SHERIA

KANISA KATOLIKI LASISITIZA HAJA YA VIONGOZI KUHESHIMU SHERIA

Kanisa limeendelea kusisitiza haja ya viongozi na asasi za serikali kuheshimu sheria. Ni maafikio yaliyotangazwa na maaskofu wa kanisa katoliki nchini Kenya mnamo tarehe 27 mei mwaka huu.

Akirejelea taarifa hiyo ya baraza la maaskofu KCCB, Askofu ya jimbo katoliki la Isiolo Antony Ireri Mukobo amesema idara zote za serikali ikiwemo mahakama, bunge na afisi kuu zinafaa kuheshimiana na kutii sheria.

Kauli ya askofu inajiri huku kukiwa na baadhi ya viongozi wanaoirushia cheche za maneno idara ya mahakama kufuatia uamuzi wa kukataa marekebisho ya katiba kuitia kura ya maoni BBI. Askofu Ireri amesema kwamba idara zote tatu za serikali zinapaswa kufanya kazi kwa pamoja na kwa uuwiano bila kuhujumiana.

Kadhalika, askofu Ireri ameshikilia msimamo wa kanisa katoliki kwamba marekebisho ya katiba yanayopendekezwa yanafaa kufanywa baada ya uchaguzi na wala si kabla yake, ili yasije yakavuruga Amani nchini.

Ameyasema haya wakati wa ibada ya misa ya jumapili. Ikumbukwe kwamba tarehe 27 mwezi uliopita kupitia taarifa ya pamoja, baraza maaskofu wa kanisa katoliki lilitoa mwelekeo kuhusu masuala kadha, yakiwemo ya uongozi, uchaguzi mkuu na kura ya maoni, janga la Korona, hali ya njaa nchini na uuwiano wa kitaifa.

RELATED ARTICLES

KWA NINI KUFUNGA MAKANISA? MAASKOFU WA KANISA KATOLIKI WALALAMIKA

Kanisa limesikitishwa na hatua ya serikali la kufunga maeneo ya ibada kila wakati kunapokuwa na mkurupuko wa virusi hivyo katika baadhi ya...

KANISA LAKASHIFU VIONGOZI KUHUSU CHECHE ZA MANENO DHIDI YA MAHAKAMA

Kanisa Alhamisi 27 Mei lilipeana wosia wake kuhusu mdahalo unaoendelea nchini baada ya uamuzi wa mahakama kuharamisha mchakato wa kuifanyia marekebisho katiba...

Kongamano:Imani na Kustawi:Mikakati ya Kuzuia na Kuponya Unyanyasaji wa Kijinsia wa Watoto

Tangu tarehe 8 -10 Aprili linafanyika Kongamano la kimataifa kwa njia ya mtandao kuhusu manyanyaso ya kijinsia kwa watoto.Tukio hili limeandaliwa na...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular

“JAMII YA AMERU ISIOLO TUSEME KWA SAUTI MOJA,’’MWENYEKITI WA NJURI NCHEKE ASEMA.

Wito umetolewa kwa jamii ya Ameru katika  kaunti ya Isiolo kudumisha amani na kutokubali kugawanyawa kwa misingi ya kimaeneo.

SENETA ABSHIRO AMTAKA MATIANG’I NA MUTYAMBAI KUTOA TAARIFA KUHUSU SHAMBULIZI ENEO LA MADOWALE.

Seneta mteule Abshiro Halakhe amemwomba waziri wa usalama na maswala ya ndani ya nchi Daktari Fred Matiangi, na inspekta generali wa polisi...

READINGS AT MASS TUESDAY 22 JUNE 2021

 12th Week in Ordinary Time Liturgical Colour: Green. First reading

St. Paulinus of Nola

22nd June Anyone who is praised in the letters of six or seven saints undoubtedly must be of extraordinary...

Recent Comments